Home » » MAKONDA APIGA MARUFUKU UVUTWAJI WA SHEESHA, USHOGA NA UVUTAJI SIGARA HADHARANI JIJINI DAR

MAKONDA APIGA MARUFUKU UVUTWAJI WA SHEESHA, USHOGA NA UVUTAJI SIGARA HADHARANI JIJINI DAR

Written By CCMdijitali on Monday, July 4, 2016 | July 04, 2016


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ametanga na kupiga marufuku uvutaji wa Sheesha katika maeneo yote ya Jiji la Dar na kutoa siku saba za kusitishwa kwa huduma hiyo ambayo imekuwa ikipatikana maeneo mengi ya burudani hapa mjini.

Makonda ameyasema hayo leo wakati wa Kongamano la Dini lililofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam akiwa ni Mgeni Rasmi. Sheesha ni nini? Sheesha ni aina ya uvutaji wa mvuke na moshi wa tumbaku inayopunguzwa kwa moto wa mkaa. Wakati mwingine inachanganywa na matunda au vitu vyenye ladha ya sukari.

Matumizi yake yalianzia mashariki ya kati lakini sasa imeenea mabara yote Duniani.

Kwa jijini Dar es salaam watumiaji wakubwa ni vijana wa kike na kiume na watu wazima, ambapo imeelezwa kuwa na Madhara kiafya kwa sababu ya sumu za aina tofauti zilizomo ndani ya moshi wa tumbaku na madawa mengine. Sheesha inaweza pelekea kupata Ugonjwa wa Saratani, magonjwa ya moyo, magonjwa ya ngozi, fizi za meno, kupugua kinga ya mwili, wajawazito kujifungua njiti na watoto wenye uzito mdogo, kuwa tegemezi na ngozi kusinyaa.

Mbaya zaidi Sasa hivi watu wanachanganya na madawa ya kulevya, ambayo ni madhara makubwa kiafya. Falme za kiarabu na nchi nyingine kama Uganda wamepiga marufuku matumizi ya Sheesha, kwani Hakuna faida yoyote ya kuvuta sheesha na inaangamiza vijana na kupunguza nguvu kazi ya taifa na kwenda kinyume na malengo ya awamu ya 5.

Sababu hizo ndiyo zimemfanya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda kutangaza kupiga marufuku uvutaji wa sheesha.




Kwa upande mwingine, Makonda amepiga marufuku ushoga kwenye mkoa wa Dar es Salaam na kuwataka mashoga wote walio kwenye Mitandao ya kijamii kama instagram na Facebook kufuta akaunti zao haraka iwezekanano la sivyo watakamatwa wote pamoja na wale wanao wa fata kwenye mitandao hiyo ya kijamii na watakuwa na hatia ile kama ya mashoga.

Pia amewapiga marufuku wavutaji wa Sigara kwenye maeneo ya wazi Jijini Dar, kwani wataalamu wanasema ule moshi wa sigara unaotoka kwa mvutaji unaweza kumuathiri zaidi yule asiyetumia Sigara kuliko yule anayetumia.

Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link