Home » » RC MAKONDA AWAAPISHWA WAKUU WAPYA WA WILAYA ZA JIJI LA DAR ES SALAAM LEO

RC MAKONDA AWAAPISHWA WAKUU WAPYA WA WILAYA ZA JIJI LA DAR ES SALAAM LEO

Written By CCMdijitali on Monday, July 4, 2016 | July 04, 2016

RC MAKONDA AWATAKA WAKUU WAPYA WA WILAYA JIJINI DAR KUJITUMA, ATAKAYESHINDWA KUTAFUTIWA WILAYA NYINGINE


Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewaagiza wakuu wapya wa wilaya za Mkoa wa Dar es salaam kufanya kazi kwa kujituma katika kuwatumikia wananchi na atakayeshindwa atamshauri Rais amtafutie wilaya nyingine.

Makonda ameyasema hayo leo wakati akiwaapisha wakuu wa Wilaya Wanne kati ya watano  katika jiji la Dar es Salaam, amesema Mkoa wake ni wenye idadi kubwa ya watu kuliko mikoa mingine hivyo kila mtu lazima afanye kazi ya kutatua changamoto zilizo mbele yake na bila kufanya hivyo nafasi ya ukuu wa mkoa itakuwa imemshinda.

Amesema kuwa wakuu wa wilaya wametakiwa kusimamia sheria ikiwa ni kupiga marufuku uvutaji wa shisha katika mkoa wa Dar es Salaam, Uvutaji Sigara hadharani na wataofanya hivyo watafikishwa katika vyombo vya sheria.

Makonda amesema kuwa operesheni ya kuondoa ombaomba bodo inaendelea na wakuu wilaya wametakiwa kusimamia operesheni hiyo kutokana na mazingira mazuri ya elimu yaliyowekwa kwa watoto hao kusoma ili waweze kuachana na utegemezi huo.

Makonda amesema kuwa watu wanaowasaidia wanaomba wanafanya makosa kwa kufanya watu hao washindwe kuondoka katika jiji la Dar es Salaam.

Aidha amesema kuwa tatizo la madawati bado lakini kuna upungufu wa vyumba vya madawati ambayo ni muhimu katika kuweza kuainisha katika kipindi hiki.

Wakuu wa Wilaya walioapishwa leo ni, Hashim Mgandilwa  wa  Kigamboni, Felix Lyaviva wa Temeke, Sophia  Mjema wa Ilala na Ally Hapi wa Kinondoni.

Mkuu wa Wilaya wa Ubungo Humphrey Polepole hajaapa kutokana na udhuru ya msiba wa baba yake mazazi ambaye ataapa baada ya kumaliza udhuru hiyo.

Wakuu wa Wilaya baada ya kuapishwa walikuwa na  maoni tofauti, kwa upande Mkuu wa Wilaya Kigamboni, Hashimu Mgandilwa amesema kuwa kazi yake ni kuitangaza Kigamboni kuwa ni Wilaya katika njia ya mbalimbali ya mawasiliano lakini sifa kwake kuanzisha Wilaya hiyo.

Naye Mkuu wa Wilaya Ilala, Sophia Mjema ambaye alikuwa ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke amesema ametangaza kiama kwa ombaomba katika jiji na kutaka maafisa Ustawi wa Jamii kufanya kazi yao na kama watashindwa atawashughulikia.

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi amesema kuwa amefanya kazi siku 74 kabla hajateuliwa na Rais ameweza kumaliza tatizo la madawati kwa Wilaya ya Kinondoni na kuahidi kuendelea na kasi yake.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akihutumia wananchi katika hafla ya  kuapishwa kwa Wakuu wa Wapya wa Wilaya za Jiji la Dar es salaam leo Julai 4, 2016.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akimuapisha Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema, katika Ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es salaam leo Julai 4, 2016.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akimuapisha Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa, katika Ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es salaam leo Julai 4, 2016.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akimuapisha Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi, katika Ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es salaam leo Julai 4, 2016.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akimuapisha Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaviva, katika Ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es salaam leo Julai 4, 2016.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akisalimiana na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, CP Simon Sirro, wakati alipowasili kwenye ukumbi wa Karimjee kulikofanyika hafla ya kuapishwa kwa Wakuu wa Wapya wa Wilaya za Jiji la Dar es salaam leo Julai 4, 2016.PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI - MMG
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es salaam, Ramadhan Madabida, wakati alipowasili kwenye ukumbi wa Karimjee kulikofanyika hafla ya kuapishwa kwa Wakuu wa Wapya wa Wilaya za Jiji la Dar es salaam leo Julai 4, 2016.
 Sehemu ya Wakuu wa Ulinzi na Usalama wa Jiji la Dar es salaam wakiwa kwenye hafla hiyo.

 Sehemu ya Wageni mbalimbali waliohudhulia hafla hiyo.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akihutumia wananchi katika hafla ya  kuapishwa kwa Wakuu wa Wapya wa Wilaya za Jiji la Dar es salaam leo Julai 4, 2016.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akimuapisha Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema, katika Ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es salaam leo Julai 4, 2016.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akisaini hati ya kiapo cha Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema mara baada ya kumuapisha, katika Ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es salaam leo Julai 4, 2016.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akimkabidhi Katiba ya nchi na Ilani ya CCM Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema mara baada ya kumuapisha, katika Ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es salaam leo Julai 4, 2016.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akimuapisha Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa, katika Ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es salaam leo Julai 4, 2016.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akimkabidhi Katiba ya nchi na Ilani ya CCM, Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa mara baada ya kumuapisha, katika Ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es salaam leo Julai 4, 2016.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akimuapisha Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi, katika Ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es salaam leo Julai 4, 2016.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akisaini hati ya kiapo cha Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi mara baada ya kumuapisha, katika Ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es salaam leo Julai 4, 2016.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda (kulia) akimkabidhi Katiba ya nchi na Ilani ya CCM, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi mara baada ya kumuapisha, katika Ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es salaam leo Julai 4, 2016.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akimuapisha Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaviva, katika Ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es salaam leo Julai 4, 2016.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akisaini hati ya kiapo cha Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaviva mara baada ya kumuapisha, katika Ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es salaam leo Julai 4, 2016.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda (kulia) akimkabidhi Katiba ya nchi na Ilani ya CCM, Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaviva mara baada ya kumuapisha, katika Ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es salaam leo Julai 4, 2016.
 Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita akiwa pamoja na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, CP Simon Sirro.

 Wakuu wapya wa Wilaya wa Jiji la Dar es salaam, toka kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema, Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaviva. Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Humphrey Polepole hakuweza kuhudhulia hafla hiyo kutokana na kupatwa na dharula. hivyo ataapishwa pindi atakapomaliza dharula yake.
 Mapitio kigo katika hati ya Kiapo.








Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link