Nangole apinga hukumu ya ubunge
Kwa ufupi
Wiki chache zilizopita, Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, Sivangilwa Mwangesi alitoa hukumu hiyo baada ya kujiridhisha na malalamiko ya Dk Stephen Keruswa
Wa CCM kwamba mazingira katika chumba cha majumuisho ya kura hayakuwa rafiki kuakisi matakwa ya wapiga kura.
By Moses Mashalla, Mwananchi mmashalla@mwananchi.co.tz
Arusha. Aliyekuwa Mbunge wa Longido (Chadema), Onesmo Ole Nangole amekata rufaa kupinga hukumu ya kuvuliwa ubunge.
Wiki chache zilizopita, Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, Sivangilwa Mwangesi alitoa hukumu hiyo baada ya kujiridhisha na malalamiko ya Dk Stephen Keruswa
Wa CCM kwamba mazingira katika chumba cha majumuisho ya kura hayakuwa rafiki kuakisi matakwa ya wapiga kura.
Ole Nangole amesema hayo alipokutana na baadhi ya wakazi wa jimbo hilo nyumbani kwake mjini Longido na kuwaelezea msimamo wake wa kukata rufaa.
“Hukumu haikuwa ya haki hata kidogo, hakuna fujo yoyote tuliyofanya sisi tulikuwa tukidai haki ya kutangaziwa matokeo na hiyo ni haki yetu,” amesema.
Amewaambia kwamba ameshawasilisha maombi ya kukata rufaa ambayo tayari yamepokewa.