Home » » UMMY MWALIMU ATEMBELEA MAKAZI YA WAZEE KIILIMA BUKOBA VIJIJIN

UMMY MWALIMU ATEMBELEA MAKAZI YA WAZEE KIILIMA BUKOBA VIJIJIN

Written By CCMdijitali on Saturday, July 16, 2016 | July 16, 2016


WAZIRI wa Afya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ameitaka jamii kujenga tabia ya kusaidia wazee ili na wao waweze kuyamudu maisha yao.

Ummy ameyasema hayo leo wakati alipotembelea makazi ya kutunzia wazee katika kituo cha kiilima kilichopo katika Wilaya ya Bukoba vijijini.kuwa wazee wametoa mchango mkubwa kwa Taifa na bado wanamchango mkubwa pia katika Taifa hivyo lazima jamii inayoishi nayo kuwatunza na kuwaheshimu.

"Wazee wangu mimi nipo pamoja na nyie,na matatizo yenu yote nimeyasikia tutaendelea kuyatatua kadri fedha zitakavyo kuwa zinapatikana"alisema.Alisema kuwa ameguswa na matatizo waliyonayo wazee hao kituoni hapo ikiwemo tatizo la huduma ya afya,vyoo,maji pamoja na makazi ya kulala.

Wazee hao walimuomba Waziri kuwekea mkazo katika suala la huduma za matibabu pamoja na usafiri wa uhakika wa kuwapelekeka hospital pale wanapouugua."Mhe.Waziri tunaomba utufanyie mpango tupate gari hapa kwenye makazi yetu la kutupeleka hospital pale tunapo umwa,hii kwetu ni changamoto kubwa hasa akitokea mgonjwa usiku"alisrma mzee Andrea Lwiza.


Waziri Ummy Mwalimu akiongea na wazee wanaotunzwa katika kituo cha kulelea wa wazee Kiilima 
Waziri wa afya jinsia maendeleo wazee na watoto akiangalia vyoo wanavyotumia wazee wanaotunzwa katika kituo cha Kiilima kilichopo Wilaya ya Bukoba  vijijini. 
 
 Baadhi ya wazee wanaotunzwa katika kituo cha kulelea wazee cha Kiilima wakimsikiliza waziri (hayupo pichani) 
Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link