Raia wa Afrika ya Kusini, Gugu Zulu (38) amefariki dunia leo baada ya kupatwa na tatizo la kushindwa kupumua kwenye mwinuko wa Mlima
Kwa ufupi
Meneja Uhusiano wa Shirika la Hifadhi za Taifa nchini (Tanata), Paschal Shelutete amesema shirika hilo kwa kushirikiana na mamlaka mbalimbali za Serikali zinaendelea na uratibu wa kurejesha mwili wa marehemu Afrika ya Kusini kwa kwa mazishi.
Dar es Salaam. Raia wa Afrika ya Kusini, Gugu Zulu (38) amefariki dunia leo baada ya kupatwa na tatizo la kushindwa kupumua kwenye mwinuko wa Mlima Kilimanjaro.
Meneja Uhusiano wa Shirika la Hifadhi za Taifa nchini (Tanata), Paschal Shelutete amesema shirika hilo kwa kushirikiana na mamlaka mbalimbali za Serikali zinaendelea na uratibu wa kurejesha mwili wa marehemu Afrika ya Kusini kwa kwa mazishi.
Shelutete amesema Zulu alifika nchini na kuanza kupanda Mlima Kilimanjaro Julai 14 kuenzi jitihada za Rais wa Kwanza wa Afrika ya Kusini, Nelson Mandela za kusaidia familia maskini nchini Afrika ya Kusini, hususani kuwapatia mahitaji muhimu watoto wa kike ambao hawana uwezo wa kupata mahitaji muhimu.
Hii ni mara ya pili kwa watalii kutoka Afrika ya Kusini kupanda Mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kuenzi juhudi za Mandela katika kusaidia jamii ya watoto wa kike.