Awamu ya kwanza ya ujenzi wa kiwanda hicho kinachomilikiwa na mwekezaji mzawa kwa kushirikiana na Wachina, inatarajiwa kukamilika Oktoba, mwaka huu na fedha hizo zitapatikana baada ya kukamilika awamu tatu za ujenzi wake.
Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda hicho, Mohammed Kilua amemweleza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuwa, ujenzi huo utasaidia kuimarisha uchumi.
Majaliwa aliyetembelea kiwanda hicho mjini Kibaha mkoani Pwani jana.
Kiluwa amesema, kiwanda hicho kitazalisha nondo kwa matumizi ya ujenzi pamoja na vifaa vingine vinavyohusiana na bidhaa za chuma.
“Lengo ni kuweza kuuza malighafi hizo kwenye viwanda vingine vya chuma nchini na nchi jirani kwa kuzingatia ubora unaokidhi mahitaji ya soko la kimataifa,” amesema.
“Katika awamu ya kwanza ya ujenzi, tunatarajia kutumia dola za Marekani milioni 40; awamu ya pili tutatumia dola za Marekani milioni 50 na dola za Marekani milioni 200 zitatumika kwenye awamu ya tatu ili kukamilishia ujenzi wa kiwanda hiki,” amesema.
Awamu ya kwanza inatarajiwa kukamilika Oktoba mwaka huu, wakati awamu ya tatu itakamilika Februari mwakani. Kikikamilika kinatarajiwa kuajiri vijana zaidi ya 500 wa Kitanzania.
Waziri Mkuu amesema, “Uwekezaji sio lazima ufanywe na watu wa nje, Watanzania wana nafasi ya kuwekeza katika sekta mbalimbali, Kiluwa amefungua njia hivyo wengine wafuate nyayo zake. Uwezo tunao na sababu ya kuwekeza tunayo, kwani tunataka tuzalishe bidhaa mbalimbali sisi wenyewe”.
Aliongeza kuwa uwepo wa kiwanda hicho katika eneo la Disunyara, Mlandizi mkoani Pwani, utawezesha kuboresha hali ya uchumi kwa wakazi wa eneo hilo na Taifa kwa ujumla, akitoa mfano kwa wakazi wa Mtwara, ambao wamenufaika kutokana na ujenzi wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote ambapo awali walikuwa wakinunua saruji kwa Sh 17,000, lakini hivi sasa wanainunua kwa Sh 7,000.
Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu ameliagiza Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) lipeleke umeme mapema kwenye eneo hilo ili kuharakisha shughuli za uwekezaji.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua kiwanda cha nondo cha Mohamed Kiluwa Group and Company cha Mlandizi Mkoani Pwani, wakati alipokitembelea Julai 12, 2016.Kulia kwake ni Mkuu wa mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarest Ndikilo na kushoto kwake ni mmiliki wa kiwanda, Mohammed Kiluwa. (PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU)
Baadhi ya wakazi wa Mlandizi mkoani Pwani waliofika kwenye kiwanda cha nondo cha Mohamed Kiluwa Group and Company Limited wakati Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipokitembelea Julai 12, 2016.
Baadhi ya wakazi wa Mlandizi mkoani Pwani waliofika kwenye kiwanda cha nondo cha Mohamed Kiluwa Group and Company Limited wakati Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipokitembelea Julai 12, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua kiwanda cha nondo cha Mohamed Kiluwa Group and Company cha Mlandizi Mkoani Pwani, wakati alipokitembelea Julai 12, 2016.Kulia kwake ni Mkuu wa mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarest Ndikilo na kushoto kwake ni mmiliki wa kiwanda, Mohammed Kiluwa.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua kiwanda cha nondo cha Mohamed Kiluwa Group and Company cha Mlandizi Mkoani Pwani, wakati alipokitembelea Julai 12, 2016.Kulia kwake ni Mkuu wa mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarest Ndikilo na kushoto kwake ni mmiliki wa kiwanda, Mohammed Kiluwa



