Home » » TIMU YA WATU 100 YAONGOZWA NA JK KUPANDA MLIMA KILIMANJARO KUCHANGISHA FEDHA KUSAIDIA WAATHIRIKA WA UKIMWI NA VIRUSI VYA UKIMWI

TIMU YA WATU 100 YAONGOZWA NA JK KUPANDA MLIMA KILIMANJARO KUCHANGISHA FEDHA KUSAIDIA WAATHIRIKA WA UKIMWI NA VIRUSI VYA UKIMWI

Written By CCMdijitali on Sunday, July 17, 2016 | July 17, 2016


Na issamichuzi.blogspot.com

Mgodi wa Dhahabu wa Geita(GGM) kwa kushirikiana na Tume ya Taifa ya Kudhibiti UKIMWI(TACAIDS) wamezindua rasmi zoezi la kupanda Mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kuchangisha fedha za kusaidia tatizo la UKIMWI na Virusi vya UKIMWI nchini. Kampeni ya kuchangisha fedha kusaidia waathirika wa UKIMWI na Virusi vya UKIMWI  kupitia upandaji Mlima Kilimanjaro hufanyika kila mwaka na mwaka huu ukiwa ni mwaka wake wa  15,Mgodi wa Dhahabu wa Geita umeratibu wapandaji 100 katika zoezi hilo.

 Akizungumza kwenye hafla ya kuwatakia heri wapandaji  wanaoanza zoezi la kupanda Mlima Kilimanjaro kwa muda wa siku saba,Mgeni Rasmi,Rais Mstaafu wa awamu ya Nne Dkt  Jakaya Mrisho Kikwete ametoa ujumbe maalumu kuhusu vita ya UKIMWI na Virusi vya UKIMWI akisema panahitajika ushirikiano wa karibu baina ya Serikali na sekta binafsi ili kupunguza tatizo hilo

Rais Kikwete amesema kuwa kupambana na UKIMWI pamoja na Virusi vya UKIMWI si jambo dogo hivyo panahitajika ushirikiano kwa Serikali na wadau wote.

Rais Mstaafu wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia hafla ya kuwaaga wapanda Mlima 100 kwenye Kampeni ya Mgodi wa Dhahabu wa Geita(GGM),Kampeni inayoratibiwa na Mgodi wa Dhahabu wa Geita kwa kushirikiana na Tume ya Kudhibiti UKIMWI(TACAIDS).Pembeni yake kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mgodi wa Dhahabu wa Geita Bw Terry Mulpeter pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Said Meck Sadique.

‘‘Serikali imeendelea kufanya jitihada nyingi kupunguza tatizo hili kwa kushirikiana na sekta binafsi kupunguza tatizo hili.Tumekuwa tukishirikiana na wadau kama Mgodi wa Dhahabu wa Geita(GGM)  kwa miaka 15 mfululizo kupunguza maambukizi mapya,vifo vitokanavyo na UKIMWI pamoja na unyanyapaa kwa waathirika wa Virusi vya UKIMWI.Tumefanikiwa  kutoka tarakimu mbili kwenda kwenye tarakimu moja’’ amesema Rais Kikwete.


Rais Kikwete ameongeza kuwa hatua ya Tanzania kufikia asilimia 5.1 ni ya kupongezwa na kwamba jamii isiridhike na hali hiyo badala yake inapaswa kuendelea kuwa makini kuchukua tahadhali dhidi ya ugonjwa huo kuanzia mtu binafsi ngazi ya familia na jamii yote kwa ujumla.
Balozi wa Kampeni ya Kili Challenge 2016, Mrisho Mpoto akitumbuiza wimbo wake wa Sauti nenda mbele ya Mgeni rasmi Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete muda mfupi kabla ya kuanza rasmi zoezi la kupanda Mlima Kilimanjaro kwa siku saba kuchangisha fedha za kusaidia waathirika wa UKIMWI na VVU nchini.

Mkurugenzi Mtendaji wa Mgodi wa Dhahabu wa Geita(GGM) Bw Terry Mulpeter amesema kuwa mwaka huu Kampeni ya Kili Challenge inahusisha wapandaji mlima 100 ambao kati yao,50 watapanda mpaka kilele cha Mlima  Kilimanjaro na 50 wataendesha baiskeli kuzunguka mlima kwa  umbali wa kilomita 380 kwa muda wa siku saba au wastani wa kilomita 60 kila siku.

Rais Kikwete ameongeza kuwa hatua ya Tanzania kufikia asilimia 5.1 ni ya kupongezwa na kwamba jamii isiridhike na hali hiyo badala yake inapaswa kuendelea kuwa makini kuchukua tahadhali dhidi ya ugonjwa huo kuanzia mtu binafsi ngazi ya familia na jamii yote kwa ujumla.


Mkurugenzi Mtendaji wa Mgodi wa Dhahabu wa Geita(GGM) Bw Terry Mulpeter amesema kuwa mwaka huu Kampeni ya Kili Challenge inahusisha wapandaji mlima 100 ambao kati yao,50 watapanda mpaka kilele cha Mlima  Kilimanjaro na 50 wataendesha baiskeli kuzunguka mlima kwa  umbali wa kilomita 380 kwa muda wa siku saba au wastani wa kilomita 60 kila siku.

Bw Terry Mulpeter ameongeza  kuwa jitihada za Mgodi wa Dhahabu wa Geita(GGM) kuchangisha fedha kupitia Kampeni ya  Kili Challenge ni za kuungwa mkono kwa kuwa zina lengo la kuboresha maisha ya waathirika wa UKIMWI na Virusi vya UKIMWI.

Mwaka huu wapandaji Mlima Kilimanjaro kupitia Kampeni ya Kili Challenge  wanatoka katika mataifa ya Tanzania, Afrika ya Kusini,Marekani,Uingereza na Australia .Mpaka sasa Kampeni ya Kili Challenge imechangisha jumla ya Bilioni 12 za Kitanzania fedha ambazo zimetolewa  kwa Taasisi  zaidi ya 30 za Serikali na  zisizo za Kiserikali.


Baadhi ya wapanda mlima kwa kutumia baiskeli kutoka Mgodi wa Dhahabu wa Geita wakijiandaa kupanda Mlima Kilimanjaro




Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link