Mkapa atimiza miaka 50 ya ndoa
Written By CCMdijitali on Saturday, August 27, 2016 | August 27, 2016
Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa wakikata keki katika hafla ya chakula cha mchana waliyoandaa baada ya Misa ya Jubilei ya Dhahabu ya ndoa yao katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam Agosti 27, 2016
HABARI
RAIS John Magufuli na mkewe Janet Magufuli ni miongoni mwa wageni mashuhuri waliohudhuria ibada ya Maadhimisho ya Jubilee ya miaka 50 ya ndoa ya Rais Mstaafu awamu ya tatu, Benjamin Mkapa na mkewe Anna Mkapa.
Misa ya maadhimisho hayo yaliyofanyika latika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Petro Oysterbay imeongozwa na Askofu Kuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo na kuhudhuriwa na maaskofu na viongozi mbalimbali wa serikali na taasisi za umma.
Wageni maarufu waliohudhuria maadhimisho hayo pamoja na Mawaziri Wakuu wastaafu wa Tanzania Cleopa Msuya, Dk Salim Ahmed Salim, Jaji Joseph Warioba, Edward Lowassa na mkewe na mjane wa baba wa taifa, mama Maria Nyerere.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Waziri Mkuu wa zamani Mhe Edward Lowassa wakati wa Misa ya Jubilei ya Dhahabu ya ndoa ya Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016
Paroko akisimamia ukumbusho wa ahadi za ndoa wakati wa Misa ya Jubilei ya Dhahabu ya ndoa ya Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam l Agosti 27, 2016
Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa wakipokea hati maalumu ya ndoa toka kwa ASKOFU Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo wakati wa Misa ya Jubilei ya Dhahabu ya ndoa ya Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam Agosti 27, 2016
Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa akitoa shukurani wakati wa Misa ya Jubilei ya Dhahabu ya ndoa yake na na Mama Anna Mkapa katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam Agosti 27, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akitoa salamu zake za pongezi wakati wa Misa ya Jubilei ya Dhahabu ya ndoa ya Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam Agosti 27, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli katika picha ya pamoja viongozi wa dini na viongozi wastaafu na wake zao wakati wa Misa ya Jubilei ya Dhahabu ya ndoa ya Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam Agosti 27, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli katika picha ya pamoja viongozi wa dini na viongozi wastaafu na wake zao na familia ya mhe Benjamin Mkapa wakati wa Misa ya Jubilei ya Dhahabu ya ndoa ya Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam Agosti 27, 2016
Katibu Mkuu wa CCM Ndg Abdulrahman Kinana akiteta jambo na Waziri Mkuu wa zamani Mhe Edward Lowassa wakati wa hafla ya chakula cha mchana baada ya Misa ya Jubilei ya Dhahabu ya ndoa ya Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam Agosti 27, 2016
Labels:
KITAIFA