Imeandikwa na Anastazia Anyimike | Habari leo
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu ( Sera, Bunge,Vijana, Kazi, Ajira na Walemavu) Jenister Mhagama akikabidhi mfano wa hundi ya mkopo ambao Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) limeutoa kwa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) kwa ajili ya kuongeza uzalishaji kwenye kiwanda cha viuadudu cha Kibaha, Pwani. Katikati ni Mwenyekiti wa Bodi wa NDC, Dk Samuel Nyantahe, kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Azania Bank, Godfrey Dimaso na Kulia ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Assumpta Mshama.
SHIRIKA la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) limelikopesha Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) dola za Marekani milioni 2.1 ambazo ni sawa na sh bilioni nne za Tanzania kuongeza uzalishaji katika kiwanda cha viuadudu kilichopo Kibaha, Pwani.
Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Profesa Godius Kahyarara amesema mkopo huo utakiwezesha kiwanda hicho kujiendesha kwa ufanisi na kuongeza usalishaji. Profesa Kahyarara amesema kiwandani hapo kuwa, mkopo huo utapitia na kusimamiwa na Benki ya Azania.
Amesema, NSSF ipo tayari kupokea maombi mengine ya mkopo kutoka NDC kwa kuwezesha masoko ya bidhaa hiyo.
“Huo ni mwanzo wa NSSF kuunga mkono katika uwekezaji kwani tunatarajia kuwekeza kuifufua shirika la usagishaji (National Millings), kiwanda kikubwa cha sukari ambacho tutakijenga kwa kushirikiana na PPF, kiwanda cha nguo, viatu na matairi,” amesema.
NDC yakopeshwa bil 4/- kukabili malaria
Written By CCMdijitali on Monday, August 29, 2016 | August 29, 2016
Labels:
BIASHARA