Kwa ufupi
Walimu na wanafunzi hao, wametajwa katika kura za siri zilizopigwa na kutokana na kuibuka matukio ya kuchomwa moto shule wilayani Monduli
Arusha. Jeshi la polisi wilayani Monduli Mkoa wa Arusha, linawashikilia kuwahoji walimu wanne na wanafunzi wanane kutokana na tuhuma za uchomaji moto Shule ya Sekondari Ole Sokoine.
Walimu na wanafunzi hao, wametajwa katika kura za siri zilizopigwa na kutokana na kuibuka matukio ya kuchomwa moto shule wilayani Monduli ambapo ndani ya mwezi mmoja shule tatu zimechomwa moto na kusababisha hasara ya Sh 215 milioni.
Mkuu wa Wilaya ya Monduli, Idd Kimanta akizungumzia walimu na wanafunzi hao alisema majina yao yanahifadhiwa wanahojiwa na polisi ili kujua kama wamehusika na uchomaji wa shule hiyo.