Home » , » MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AFUNGUA MKUTANO WA WAKUU WA MAJESHI YA POLISI WA NCHI ZA KUSINI MWA AFRIKA (SARPCCO)

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AFUNGUA MKUTANO WA WAKUU WA MAJESHI YA POLISI WA NCHI ZA KUSINI MWA AFRIKA (SARPCCO)

Written By CCMdijitali on Friday, September 16, 2016 | September 16, 2016

 Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan (kulia) akihutubia wakati wa Ufunguzi wa mkutano wa Wakuu wa Majeshi ya Polisi kutoka nchi za Kusini mwa Afrika (SARPCCO) kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa AICC jijini Arusha.

 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Ernest Mangu ambaye amekabidhiwa Uenyekiti wa Shirikisho la Wakuu wa Majeshi ya Polisi Kusini mwa Afrika (SARPCCO) akipeana mikono na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Msumbiji Dos Santos JANE (kushoto) ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Shirikisho hilo mara baada ya kukabidhiana Uenyekiti katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa AICC jijini Arusha.

 Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan (kulia) akimpa mkono wa pongezi Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Ernest Mangu mara baada ya kukabidhiwa Uenyekiti wa SARPCCO kwenye mkutano wa Wakuu wa Majeshi ya Polisi wa Nchi za Kusini mwa Afrika.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Hamad Masauni akihutubia kwenye mkutano wa Wakuu wa Majeshi ya Polisi wa nchi za kusini mwa Afrika.


..........................................................................

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewataka Wakuu wa Majeshi ya Polisi Kusini mwa Bara la Afrika kuweka mipango na mikakati madhubuti ya kukabiliana na vitendo mbalimbali vya uhalifu vinavyotokea katika ukanda huo kama hatua ya kuhakikisha wananchi wanafanya kazi zao kwa amani na utulivu.

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo 16-Sep-2016 wakati anafungua mkutano wa Wakuu wa Majeshi ya Polisi Kusini mwa Afrika katikaukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC jijini Arusha.

Makamu wa Rais amesisitiza kuwa anaimani kubwa kuwa mkutano huo utakuwa ni chachu katika kuibua changamoto mbalimbali za kihalifu na kuzifanyia kazi ipasavyo kwa manufaa ya ukanda huo.

Amesema ni wajibu wa wakuu hao wa majeshi ya polisi ya kusini mwa Afrika kujiepusha na malalamiko yasiyo ya msingi kutoka kwa raia ambayo yanasababishwa na vitendo vya urasimu, uzembe na rushwa ili kujenga uwazi na uwajibikaji.Makamu wa Rais pia amehimiza kudumishwa kwa ushirikiano miongoni mwa wakuu wa majeshi ya polisi kusini mwa Afrika katika kubadilishana mbinu bora za kukabiliana na vitendo vya uhalifu wa kuvuka mipaka.

Katika mkutano huo Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini –IGP- Ernest Mangu amekabidhiwa uenyekiti wa Shirikisho la wakuu wa Majeshi ya Polisi kusini mwa Afrika (SARPCCO) kutoka kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi wa Nchi ya Msumbiji Dos Santos JANE.

Shirikisho la SARPCCO lilianzishwa mwaka 1995 kwa lengo la kuimarisha ushirikiano wa majeshi ya polisi kusini mwa Afrika katika kukabiliana na vitendo  vya  uhalifu katika ukanda huo.

Shirikisho hilo linaundwa na nchi wanachama 15 ambapo baadhi ya nchi hizo ni Angola, Botswana, Msumbiji, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo- DCR-,Malawi, Zambia, Zimbabwe, Madagascar,Swaziland, Afrika Kusini,Lesotho,Syshelles na Tanzania ambayo ni mwenyekiti mpya wa SARPCCO.

Tanzania imekabidhiwa uenyekiti wa SARPCCO wakati ndio Mwenyekiti mpya wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika inayojulikana kwa jina la (SADC TROIKA).

























Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link