Mufti Mkuu wa Tanzania,Sheikh Aboubakary Zubery |
Kwa ufupi
Kauli hiyo ya Mufti Zubery imetangazwa leo na Sheikh Mkuu wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum wakati kikao cha kuwatambulisha safu ya viongozi wapya wa Baraza la Vijana la Jumuiya ya Waislamu wa Dar esSalam.
Dar es Salaam. Mufti Mkuu wa Tanzania,Sheikh Aboubakary Zubery ametangaza Septemba 12 mwaka huu kuwa ndiyo siku ya Sikukuu ya Eid Alhaj itakayoswaliwa kitaifa katika makao makuu ya Baraza la Waislam Tanzania (Bakwata).
Kauli hiyo ya Mufti Zubery imetangazwa leo na Sheikh Mkuu wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum wakati kikao cha kuwatambulisha safu ya viongozi wapya wa Baraza la Vijana la Jumuiya ya Waislamu wa Dar esSalam.
Mufti Zubery amesema sikukuu itakuwa Septemba 12 baada ya mwezi kuandamana jana hivyo leo ni mwezi mosi kwa lugha ya kiarabu.