Kwa ufupi
- Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania, Mohamed Mpinga, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.
By Lilian Timbuka, Mwananchi
Dar es Salaam. Basi la Kampuni ya New Force lililokuwa likitokea Dar es Salaam kuelekea Songea, limepata ajali jioni hii eneo la Kifanya mkoani Njombe.
Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania, Mohamed Mpinga, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.
Hata hivyo, amesema taarifa kamili ya madhara ya ajali itatolewa baadaye. “Hivi ninavyozungumza na wewe, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe na RTO wake wako kwenye eneo la tukio,” amesema Mpinga
Taarifa aliyoitoa Mbunge wa Songwe, Philip Mulugo kwenye moja ya mtandao wa kijamii aliyeshuhudia ajali hiyo alipkuwa akipita kuelekea Songea, amesema huenda kukawa na idadi kubwa ya majeruhi kwani mpaka anaondoka eneo la ajali, baadhi ya abiria waliokuwa kwenye basi hilo walikuwa hawajatolewa na walikuwa wamebanwa na vyuma. “Tumefanikiwa kuwachomoa maiti kadhaa, lakini madhara huenda ni makubwa,” amesema Mulugo.