Home » » Waalimu waliokuwa wakidai fedha Jiji la Arusha 701 walipwa wote milioni 169 ARUSHA

Waalimu waliokuwa wakidai fedha Jiji la Arusha 701 walipwa wote milioni 169 ARUSHA

Written By CCMdijitali on Friday, September 23, 2016 | September 23, 2016


Picha za Waalimu walioudhuria mkutano  wa MKUU wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo uliofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa AICC uliopo mkoani Arusha Sept 20, 2016



Idadi ya waalimu waliokuwa wakidai  fedha kwa jiji la Arusha imefikia 701 ambapo  leo september 23 imeeleza kulipwa  wote milioni 169  

Mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqaro akizungumza na vyombo vya habari amesema fedha zote zimekwisha lipwa kwa wakati na hakuna mwalimu yeyote anayedai katika jiji la Arusha

Gabriel amesema serikali ya awamu ya tano imejipanga katika kuhakikisha inasimamia masuala yote ya msingi ikiwemo waalimu ambao wamekuwa wakihangaika kutafuta stahiki zao nakutekeleza agizo la mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo lililotaka  waalimu kulipwa

Ameongeza kwamba baada ya mkuu wa mkoa kuwabana madiwani ambao walikuwa wakijilipa fedha  kinyume na utaratibu zimepatikana na kupelekea waalimu kulipwa.
Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link