Home » » Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akutana na Mabalozi na taasisi mbalimbali kuchangia maafa ya tetemeko la ardhi Kagera

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akutana na Mabalozi na taasisi mbalimbali kuchangia maafa ya tetemeko la ardhi Kagera

Written By CCMdijitali on Tuesday, September 13, 2016 | September 13, 2016



Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameongea na Mabalozi na Wawakilishi wa wafanyabishara Ikulu jijini Dar es Salaam kutoa taarifa ya tatemeko la ardhi na maafa yaliyotokana tarehe 10 September 2016.

Waziri Majaliwa amewaomba wawakilishi hao kutoa misaada mbalimbali ili kuungana na Serikali kuwasaidia walioathirika mkoani Kagera.

Baadhi ya Taasisi na Balozi zilizo ahidi kutoa michango ni:-
  • Ubalozi wa China – Milioni 100
  • Ubalozi wa Kuwait – Euro 10,000
  • Ubalozi wa Kenya- wametoa mabati na malazi
  • Kampuni ya China Mercharnt Group – Mil 100
  • Mo Dewji – Milioni 100
  • Toyota Ltd – Milioni 10
  • TBL – Milioni 100
  • Woolworth -Milioni 20
  • Sahara Tanzania – Milioni 20
  • Azania Group – Milioni 20
  • Kagera Sugar -Milioni 100 na Tani 10 za sukari
  • Nosime Group- Milioni 75
  • Tanga Cement – Mifuko 1000 ya Saruji
  • Reginald Mengi – Milioni 110
  • Protas Ishengoma- Wakili na mhanga wa tetemeko Milioni 5
  • GBP, MOIL,&OILCOM- Watajenga shule mbili zilizoharibika

Vile vile Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje ametangaza matembezi ya kukumbuka janga hilo na kuahidi wananchi wote na mashirika mbalimbali kujitokeza katika matembezi hayo yatakayo fanyika siku ya Jumamosi asubuhi katika maeneo ya Masaki.

Dar es Salaam. Shilingi 1.4 bilioni zimekusanywa katika harambee iliyoandaliwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ili kusaidia waliopata maafa ya tetemeko la ardhi mkoani Kagera Jumamosi iliyopita.

Kiasi hicho ni fedha taslimu na ahadi ambazo zimetolewa na wafanyabiashara na mabalozi wanaoziwakilisha nchi mbalimbali nchini.

Miongoni mwa wafanyabishara hao ni Kampuni za GBP, Oilcom na Moil ambazo kwa pamoja zimeahidi kukarabati shule za sekondari za Ihungo na Nyakato ambazo tayari zimefungwa.

Baadhi ya mabalozi na wafanyabiashara wameahidi kutoa fedha taslimu, mabati, saruji, vyakula na nguo.

Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link