Mwenyekiti wa Wazazi Wilaya ya Arusha mhe. Ally Mtumwa akijihabarisha muda mfupi kabla ya kuanza kwa kikao cha dharura cha Kamati ya Utekelezaji wazazi wilaya ya Arusha.
Mwenyekiti wa WAZAZI Wilaya ya Arusha Ndg. Ally Mtumwa kushoto na Katibu wa WAZAZI Ndugu Mohamed Mavallah wakielekezana jambo muda mfupi kabla ya kuanza kikao cha dharura cha Kamati ya Utekelezaji leo tarehe 8/10/2016.
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji yaWAZAZI Wilaya ya Arusha wakiwa makini kusikiliza maeelezo ya Katibu wa WAZAZI Wilaya (hayupo pichani) wakati wa kikao cha kamati ya utekelezaji.
Katibu wa WAZAZI Wilaya ya Arusha Ndugu Mohamed Mavallah aliyesimama akitoa maelezo ya kumkaribisha Mwenyekiti wa WAZAZI Wilaya kufungua kikao cha Kamati ya Utekelezaji Wilaya ya Arusha.
Kikao cha Kamati ya Utekelezaji WAZAZI Wilaya ya Arusha kikiendelea.
Picha zote na Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Wilaya ya Arusha .
KAMATI YA UTEKELEZAJI YA JUMUIYA YA WAZAZI WILAYA YA ARUSHA YAKUTANA KUJADILI MAENDELEO YA UTEKELEZAJI YA MPANGO KAZI WA MIEZI MITATU KUANZIA OKTOBA 01, HADI DESEMBA 31,2016.
Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Arusha leo tarehe 08/10/2016 imefanya kikao chake cha dharura kujadili maendeleo ya MPANGO KAZI wao wa miezi mitatu kuanzia Oktoba 01, 2016 hadi Desemba 31, 2016. Katika kikao hicho wajumbe walijadiliana kupata mbinu ya kufanikisha mipango yao ikiwemo kupata pesa za kuwezesha ufanyikaji wa ziara ya Kamati ya Utekelezaji, Baraza kuu la Wilaya ambalo linatarajiwa kufanyika tarehe 29/10/2016 na Mkutano Mkuu wa Wilaya unaotarajiwa kufanyika mapema mwezi Desemba.
Sote tunaamini, WAZAZI NDIYO MSINGI IMARA WA JAMII ILIYO BORA. Tushirikiane Pamoja!
Uchungu wa Mwana, Aujuaye Mzazi.
Oktoba 08,2016