Mfalme Mohammed VI wa Morocco
Kwa ufupi
Mfalme Mohammed aliwasili jana saa 11:15 jioni akiwa na ujumbe wake wa watu zaidi ya 150, wakitokea nchini Rwanda, huku ulinzi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), ukiimarishwa.
Dar es Salaam. Mfalme Mohammed VI wa Morocco Mfalme anatarajiwa kufanya mazungumzo na Rais John Magufuli leo Ikulu jijini Dar es Salaam.
Mfalme Mohammed aliwasili jana saa 11:15 jioni akiwa na ujumbe wake wa watu zaidi ya 150, wakitokea nchini Rwanda, huku ulinzi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), ukiimarishwa.
Mambo yatakayojadiliwa na viongozi hao ni uhusiano baina ya nchi zao na Morocco kutafuta uungwaji mkono ili irejee kwenye Umoja wa Afrika (AU).
Mfalme huyo atafanya ziara rasmi ya siku tatu na baadaye ataanza likizo yake na kutumia siku tano zaidi kutembelea vivutio vya utalii.
Awali, Waziri wa Mambo ya Nje, Dk Augustine Mahiga alinukuliwa akisema msafara wa Mfalme huyo ulitanguliwa na ndege mbili zilizobeba vitu mbalimbali kwa ajili ya matumizi yake kwa kipindi chote atakachokuwapo nchini.