- Kero ya Maji yajitokeza
- Wazee waomba kupatiwa kadi za Bima ya Afya
- Wananchi walalamika kukosa huduma kwenye Zahanati ya Elerai siku za Jumamosi na Jumapili na nyakati za usiku.
- Wakala wa ukusanyaji taka (Kimbute) walalamikiwa.
- Viongozi wa Chama walalamikiwa.
Viongozi wa Wilaya waahidi kuzitafutia majibu kero hizo.
Katibu wa CCM Wilaya ya Arusha Ndg Feruzy Bano akijibu baadhi ya kero zilizowasilishwa kwenye Mkutano wa wananchi wa Mtaa wa Shams ,ulioandaliwa na Balozi wa Shina hilo Mama Maeda,kwa ajili kusikiliza matatizo yao na kuyapatia majibu. Katika Mkutano pia alikuwepo Katibu wa Siasa na Uenezi Ndg Jasper Kishumbua (aliyevaa t-shirt ya njano)
Balozi / Mwenyekiti wa Shina Mama Faustina E. Maeda (katikati) ,kulia ni Mjumbe wa Kamati ya Uongozi ya Shina Bi Joyce Edward na Mwenyekiti wa Mtaa wa Ngurumo Ndg Abubakari Jumbe wakiwa katika kikao na Wananchi wa Shina la Shams ,Mtaa wa Shams ,Kata ya Elerai katika mkutano wa Wananchi na Viongozi wa CCM Wilaya ya kufafanua na kuelezea mambo mbali mbali na kusikiliza matatizo yao na kuyatafutia majawabu .Kama inavyoelekezwa kwenye Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu mwaka 2015 ,Ibara 185 (b).
Baadhi ya Wazee Maarufu waliohudhuria katika Mkutano huo,akiwemo Mzee Ngurumo (alivaa miwani) na wazee wengine,wakifuatilia kwa makini majibu yaliyokuwa yanatolewa na Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Wilaya ya Arusha Ndg Jasper Kishumbua (hayupo katika picha).
Baadhi ya Wananchi waliohudhuria katika Mkutano huo,wakifuatilia kwa makini majibu yaliyokuwa yanatolewa na Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Wilaya ya Arusha Ndg Jasper Kishumbua (hayupo katika picha).