Na Amina Kibwana, Globu ya Jamii.
WIZARA ya Afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto imepokea vifaa vya huduma za macho vyenye thamani ya milioni 321, 234,002 kutoka kwa Shirika la Christian Blind Blind Mission kupitia benki ya Standard Chartered kupitia mradi wa "Seeing is Believing, Child Eye Health" jijini Dar es salaam.
Akipokea misaada hiyo, Waziri wa Afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto Ummy Mwalimu ameshukuru kwa msaada huo kwani kupata vifaa hivyo vitasaidia katika uboreshaji wa afya ya macho hususani kwa watoto ambapo vitazuia ulemavu wa kutokuona.
Ummy amesema kuwa, vifaa hivyo vitaboresha huduma za macho na jamii nzima itanufaika kwa uwepo wa vifaa hivi kwani matumizi yake hayataishia kwa watoto tu bali hata watu wazima wanaokabiliwa na matatizo ya macho.
"vifaa hivi vitasambazwa katika sehemu tofauti nchini na vitawalenga watu wote sio watoto tu, hii ni kutokana na kutaka kupunguza athari za magonjwa ya macho kwani hupelekea kuleta ulemavu kwani kulingana na mahitaji kuwa mengi husuani kwa watoto huduma hizi hazijafikia kiwango kinachoshauriwa na Shirika la Afya duniani,"amesema Ummy.
Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered Sanjay Rughani amesema kuwa wametoa vifaa hivyo kwa ajili ya kuwasaidia watu wote wenye matatizo ya macho wakiwemo watoto kwani wanaamini kuwa macho ni kiungo muhimu sana kwa binadamu.
Vifaa hivyo ambavyo vitagawanywa sehemu mbalimbali ikiwemo hospitali na Mikoani kama Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Hospitali ya Rufaa ya kanda Bungando,Hospitali ya Rufaa ya kanda Mbeya,Hospitali za Rufaa za mikoa ya ilala,Kinondoni,temeke,Mbeya,Rukwa,manyara,Tabora,Mwanza na Halmashauri za miji ya mbeya na babati pamoja na Halmashauri za Wilaya za Babati, Mbulu, Simanjiro,Kiteto,Igunga,Sikoine na Nzega.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Ummy Mwalimu akimkabidhi Kifaa cha uchunguziwa macho Kaimu Mganga Mkuu wa mkoa Dkt. Daisy Majamba kulia wakati wa kukabidhiana vifaa vya uchunguzi wa macho vyenye thamani ya shilingi milioni 320 leo jijini Dar es salaam.
Waziri waAfya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Ummy Mwalimu kulia akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani wakati wa kukabidhiana vifaa vya uchunguzi wa macho vyenye thamani ya shilingi milioni 320 leo jijini Dar es salaam.