Home » » Majaliwa aagiza uhakiki ya mifugo nchi nzima

Majaliwa aagiza uhakiki ya mifugo nchi nzima

Written By CCMdijitali on Saturday, December 17, 2016 | December 17, 2016

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Londoluo waliosimamisha msafara wake akiwa njiani kutoka Loliondo kwenda Longido mkoani Arusha jana. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

 
Imeandikwa na Veronica Mheta, Ngorongoro - Habari Leo

WAKUU wa Wilaya nchini wameagizwa kuhakiki idadi ya mifugo waliyonayo kwenye wilaya zao hadi ifikapo Aprili, mwakani.

Maagizo hayo yaliyotolewa juzi na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipokuwa akizungumza na wananchi waliohudhuria mkutano wa hadhara kwenye viwanja vya Waso wilayani hapa.

Pia ameitoa siku 30 kwa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) kuhakiki mpaka wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti unaopakana na vijiji vya tarafa ya Loliondo.

Alisema serikali imetoa agizo hilo kwa wakuu wa wilaya zote nchini ili iweze kujua idadi ya mifugo ambayo nchi inayo kwa kila wilaya na kupanga jinsi ya kuchanja mifugo ili isikumbwe na magonjwa mbalimbali.

Alisema hivi sasa mifugo inasumbua, mingine inaingia kwenye hifadhi mbalimbali huku mingine ikiibua migogoro kati ya wakulima na wafugaji, hivyo hivi sasa serikali inataka kudhibiti migogoro ya wakulima na wafugaji.

“Wakuu wote wa wilaya hakikisheni hadi Aprili mwakani muwe mmekamilisha uhakiki wa mifugo na nyie Tanapa mpime eneo la mpaka wa Serengeti na vijiji vya Loliondo,” alisema.


Waziri Mkuu alisema mifugo hiyo ikihakikiwa itasaidia halmashauri nchini kuhudumia mifugo kwani hivi sasa wafugaji hawaoni umuhimu wa kuchanja mifugo yao.

Naye Mbunge wa Ngorongoro ambaye ni Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, William ole Nasha alimshukuru Majaliwa kufika katika jimbo hilo na kujionea kero kubwa ya ardhi ambayo inawasumbua wananchi.

Alisema mgogoro wa pori tengefu la Loliondo umesababisha yeye kama mbunge kuchafuliwa kwenye mitandao ya kijamii na baadhi ya vyombo vya habari.




Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link