![]() |
John Minja |
Rais John Magufuli amekubali na kuridhia ombi la kusitisha mkataba na kustaafu kwa Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini Kamishna Jenerali wa Magereza (CGP) John Minja kuanzia leo.
Taarifa ya Ikulu jijini Dar es Salaam imesema Rais Magufuli amempongeza Kamishna Jenerali wa Magereza Mstaafu John Minja kwa utumishi wake na amemtakia maisha mema ya kustaafu.
Wakati huo huo, Rais Magufuli amemteua Kamishna wa Magereza (CP) Dkt. Juma Malewa kuwa Kaimu Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini hadi hapo uteuzi wa Kamishna Jenerali wa Magereza utakapofanyika.