Kwa ufupi
Lema aliyekamatwa Novemba 2, akiwa mjini Dodoma tangu wakati huo anashikiliwa kwenye gereza la Kisongo jijini Arusha.
By Mwandishi Wetu,Mwananchimwananchipapers@mwananchi.co.tz
Arusha. Sasa ni dhahiri kwamba Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema atasherehekea mwaka mpya akiwa gerezani baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Arusha kuahirisha shauri lake hadi Januari 4 mwakani.
Shauri hilo limeahirishwa leo, baada Jamhuri kuwasilisha tena notisi ya kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, kumuongezea muda wa kukata rufaa ili apate dhamana.
Desemba 20, 2016, Jaji wa mahakama hiyo, Dk Modesta Opiyo alitupilia mbali hoja za Jamhuri na kukubali maombi ya mawakili wa Lema ya kuongezewa muda wa kukata rufaa kuomba dhamana lakini leo yalishindwa kusikilizwa kutokana na Jamhuri kuwasilisha nia ya kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo.
Kesi hiyo iliyokuwa mbele ya Jaji Salma Maghimbi, upande wa Jamhuri uliwakilishwa na Mwanasheria Mwandamizi, Innocent Njau na wa Lema walikuwapo mawakili watano; Peter Kibatala, John Mallya, Adam Jabir, Faraji Mangunga na Sheck Mfinanga...