Home » » WAZIRI MKUU MGENI RASMI MAULID KITAIFA SINGIDA

WAZIRI MKUU MGENI RASMI MAULID KITAIFA SINGIDA

Written By CCMdijitali on Sunday, December 11, 2016 | December 11, 2016


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye Siku ya Maulid ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) ambayo kitaifa itaadhimishwa mkoani Singida.
Katibu wa Bakwata Mkoa wa Singida, Alhaji Buruhani Mlau alisema sherehe za Kitaifa za Maulid ya Mtume Mohammad (SAW) kwa mwaka huu zinatarajiwa kufanyika Mkoani Singida katika Kijiji cha Shelui, wilayani Iramba, Singida.
Wiki iliyopita, akitangaza utaratibu wa sherehe hizo, Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir alisema kwa mwaka huu, Maulid itasomwa usiku wa Desemba 11 na mapumziko yatakuwa siku inayofuata yaani Desemba 12.
Mufti wa Tanzania aliwataka Waislamu wote nchini waadhimishe Siku ya Maulid kwa kufanya usafi, kupanda miti na kuchangia damu. “Waislamu wanatakiwa kutumia siku hiyo kwa kufanya matendo mema na yenye kumpendeza Mwenyezi Mungu ikiwa ni pamoja na kufanya usafi kwenye mitaa yao na kuchangia damu ili kusaidia wenye uhitaji huo,” alisema.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
S.  L. P. 3021,
11410 DAR ES SALAAM.
JUMAMOSI, DESEMBA 10, 2016.(P.T)

Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link