Home » » Waziri Muhongo afungua Mkutano wa Kikanda wa Nishati Endelevu kwa Wote uliofanyika Jijini Dar es Salaam.

Waziri Muhongo afungua Mkutano wa Kikanda wa Nishati Endelevu kwa Wote uliofanyika Jijini Dar es Salaam.

Written By CCMdijitali on Monday, December 5, 2016 | December 05, 2016

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

SERIKALI kwa kupitia Waziri wa Nishati na Madini, Mh Sospeter Muhongo, imesema itaendelea kufanya kazi kwa bidii ya kusambaza umeme ili kufikia malengo ya Dunia kuhakikisha kwamba ifikapo mwaka 2030 Watanzania wote waweze kupata nishati hiyo muhimu.Waziri Muhongo aliyasema hayo wakati akifungua Mkutano wa Kikanda wa Nishati Endelevu kwa Wote uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.

Alisema usambazaji wa umeme umefanyika kwa kiasi kikubwa lakini bado wanaendelea na miradi ikiwa na lengo la kuwapatia wananchi nishati kwa uhakika kutokana na vyanzo vya nishati vilivyopo hapa nchini.

Profesa Muhongo amesema mradi wa usambazaji wa umeme vijijini umerahisisha upatikanaji wa maendeleo ya haraka kwa Watanzania wengi, hususan wale wanaoishi maeneo ya vijijini ambayo serikali imeendelea kuweka mkazo wa kufikisha huduma hiyo.

Naye Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa, Alvaro Rodriguez, alisema kukosekana kwa nishati ya umeme wa uhakika duniani kwa nchi masikini kunawafanya wananchi wakose huduma muhimu kama vile elimu afya pamoja na kufifisha maendeleo ya ukuaji wa sekta binafsi.

Aidha Rodriguez alisema Umoja wa Mataifa utaendelea kuwezesha nchi zinazoendela ikiwemo Afrika kuwezesha kifedha katika upatikanaji wa nishati ya umeme ili kuweza kufikia lengo la Dunia 2030.

MWISHO


 Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akizungumza katika ufunguzi wa mkutano wa Kikanda wa Nishati Endelevu kwa Wote uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.

 Sehemu ya washiriki wa mkutano wa Kikanda wa Nishati Endelevu kwa Wote uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akiwa kwenye picha ya pamoja na washiriki wa mkutano huo.


Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link