KWA
MWAKA WA FEDHA WA 2016/2017 PEKEE VIMEAHIRISHWA VIKAO 5 KUTOKANA NA MADIWANI.
KUGOMA KWA MADAI YA KUINGILIWA NA KUBURUZWA NA SERIKALI KUPITIA MKURUGENZI WA
JIJI.
WAFANYA BARAZA LA KUFUNGA MWAKA BILA TAARIFA ZA ROBO YA 3 NA YA 4 KWA KUGOMEA VIKAO HIVYO KWA LENGO LA KUIKOMOA SERIKALI.
Msuguano mkali kati ya madiwani na serikali kuu unazidi kupamba moto ambapo Madiwani wa Jiji la Arusha wamelazimika kufanya baraza la kufunga mwaka mnamo 29 Julai 2017 huku kukiwa hakuna mihutasari wala taarifa za:
- ·Robo ya 3 (Januari hadi Machi 2017)
- ·Robo ya 4 (April hadi Juni 2017) za kamati nyeti ya fedha na utawala.
- ·Vilevile vikao viwili vya baraza vilivunjika cha robo ya kwanza na kingine cha baraza maalum vyote kutokana na vurugu na kushutumiana kati ya Wajumbe na Mkurugenzi wa Jiji Athumani Kihamia kwa tuhuma za kutoheshimiana hasa katika maamuzi wanayoyatoa wakidai kinachotekelezwa kwa kiasi kikubwa ni maamuzi ya mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo na Mkuu wa Wilaya ya Arusha Gabriel Daqqaro badala ya maamuzi ya madiwani ambapo ilibaki kidogo ngumi zichapwe katika baraza maalum.
- ·Pia kikao cha robo ya 2 ya kamati ya mipango miji kilivujika kwa madai ya kuingiliwa kiutendaji na ofisi ya RC tuhuma hizi zilitolewa na mbunge Godbless Lema.
1. Baraza la robo ya I lilivunjika baada ya wajumbe wengi kutoka ukumbini na kukimbilia mahakamani kusikiliza kesi ya mbunge.
2. Baraza maalum lilivunjika baada ya diwani mmoja kumporomoshea matusi mkurugenzi wa jiji ambapo ilibaki kidogo zipigwe kavukavu na madiwani wengi waliposimama kama ishara ya kumvamia mkurugenzi ndipo mkurugenzi huyo akalazimika kukimbia ukumbini kukwepa kipigo hata hivyo ilibidi kikao kirudiwe chini ya usimamizi wa katibu tawala wa mkoa yeye mwenyewe mhe Richard Kwitega ambapo kiliisha kwa mbinde na mkurugenzi siku hiyo hakuhudhuria aliwakilishwa na mhandisi wa jiji.
3. Kamati ya mipango miji ilivunjwa na mbunge akidai mpaka RC atakapoacha kuingilia masuala ya hospitali inayojengwa na ya wafadili ajenda ambayo haikuwa na uhusiano na kikao hicho.
4. Kamati ya fedha robo ya 3 wajumbe walitoka ukumbini na kwenda polisi kufuatilia dhamana ya meya aliyekuwa anashikiliwa na jeshi hilo kwa kosa la kufanya mkusanyiko usiokubalika katika shule ya luck vicent akidai anapeleka rambirambi.
5. Kamati ya fedha ya robo ya 4 walikataa mjadala wakidai wanataka kwanza wakae cha robo ya 3 ambacho wanasahau kwamba walikigomea.
Vikao vyote hivyo 5 vilivunjika bila sababu inayokubalika kikanuni.
SWALI: JE MEYA WA JIJI LA ARUSHA ANA HAKI YA KUJIITA MEYA BORA KWA VURUGU HIZI ZA MADIWANI MEYA, NA MBUNGE?
Licha ya kuvunjika vikao hivi hata ambavyo vimemalizika bado kumekuwa na mivutano mikali kati ya madiwan kwa upande mmojai na mkurugenzi na wakuu wake wa idara kwa upande mwingine..
Mvutano huu ulisababisha ofisi ya rais TAMISEMI kuunda tume kuchunguza na kisha kutoa maelekezo kwa meya na mkurugenzi ambao ni viongozi wa pande zinazovutana lakini haikusaidia kwa kuwa meya hana ubavu wa kumpinga mbunge.