Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selamani Jafo akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Ruvu wakati alipotembelea shule hiyo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selamani Jafo katika picha ya pamoja na walimu wa Shule ya Sekondari ya Ruvu wakati alipotembelea shule hiyo. ......................................................................................................
Nteghenjwa Hosseah,Kibaha.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Selemani Jafo amemtaka atakayepewa jukumu la ukarabati wa Sekondari ya Ruvu wafanye kazi kwa kasi na haraka ili kuboresha mazingira ya shule hiyo.
Jafo aliyasema hayo leo asubuhi katika shule ya sekondari Ruvu iliyopo mkoani pwani ambapo ni siku ya pili tokea shule zianze kufunguliwa kwa mwaka huu 2018.
Ikumbukwe kwamba Waziri Jafo alitumia siku ya kwanza ya tarehe 08 January ya kufunguliwa shule hapa nchini kwa kuongea na wanafunzi wa mkoa wa mbeya kupitia shule ya sekondari Ilomba iliyopo jiji la Mbeya.
Jafo amesisitiza kwamba Serikali imeamua kufanya ukarabati wa Shule zote kongwe hapa nchini kupitia TEA ili kutengeneza mazingira bora ya kujifunzia na kufundishia.
Amesisitiza kwamba Serikali inayo ongozwa na Rais Dkt. John Magufuli imedhamiria kuleta mapinduzi makubwa katika elimu hapa nchini.
Jafo amewaeleza wanafunzi na walimu wa Ruvu sekondari kwamba wakati wa zoezi la ukarabati atatumia muda mwingi kukagua ujenzi wa shule hiyo akiwa pamoja na mbunge wa Jimbo hilo Mhe. Hamood Abuu Jumaa ili thamani ya fedha ipatikane.
Wanafunzi wa Ruvu sekondari walionyesha furaha kubwa kwa mipango ya Serikali juu ya shule yao kwani uchakavu wa miundombinu umekuwa ukiwaletea shida kubwa kutokana na maeneo mengi ya majengo yao kuvuja wakati wa Mvua.
Pia walimu na wanafunzi wa Shle hiyo wameahidi matokea mazuri zaidi katika mitihani inayokuja kwa kuzingatia mangira bora ya kujifunzia na kujisomea watakayokuwa wameyapata baada ya Ukarabati huo.