Home » » MAVUNDE AWAASA ASKARI WA JESHI LA POLISI KUCHANGAMKIA FURSA ZA KIUCHUMI DODOMA

MAVUNDE AWAASA ASKARI WA JESHI LA POLISI KUCHANGAMKIA FURSA ZA KIUCHUMI DODOMA

Written By CCMdijitali on Tuesday, January 9, 2018 | January 09, 2018


 Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Anthony Mavunde akizungumza katika semina fupi ya Chama cha Polisi Wanawake.

 washiriki wa semina

 


washiriki wa semina

 
Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Anthony Mavunde amewataka askari wa kike wa Jeshi la Polisi mkoani Dodoma kuchangamkia fursa za kiuchumi zilizopo mkoani hapo kwa kushiriki katika shughuli mbalimbali za uzalishaji mali na uchumi wa viwanda.

Mavunde ameyasema hayo leo wakati akizungumza na Chama cha Polisi Wanawake katika semina fupi aliyoiandaa katika Bwalo la Polisi-Dodoma kwa lengo la kuwapa Askari Polisi elimu juu ya masuala ya UJASIRIAMALI na UWEKEZAJI.


“Najua jukumu lenu la msingi ni Ulinzi wa Mali na Raia,lakini si vibaya pia mkautumia muda wenu wa ziada kufanya shughuli za uzalishaji mali kwa lengo la kuwaongezea kipato”amesema Mavunde

Naye,Kiongozi wa mtandao wa Askari Polisi wanawake Mkoa wa Dodoma SP Hiki amemshukuru Mbunge Mavunde kwa kuona haja na umuhimu wa kukutana na Askari hao na kufanikisha semina hiyo ambayo imehusisha wataalamu kutoka SIDO,Mifuko ya Uwezeshwaji na Wataalamu kutoka Manispaa ya Dodoma.


Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link