Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo na baadhi ya viongozi wa TAFOPA ofisini kwake mapema leo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo katika Picha ya pamoja na viongozi wa TAFOPA.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo(kushoto) akiagana na Mwenyekiti wa TAFOPA Suzy Laiser mara baada ya kikao chao mapema leo.
Nteghenjwa Hosseah,Dar es Salaam
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa amepongeza Umoja wa Washindaji wa Vyakula(Tafopa) kwa jitihada zao za kuunga mkojo kampeni ya ujenzi wa viwanda 100 kila Mkoa inayojulikana kama Mkoa wangu Viwanda vyetu.
Waziri Jafo ametoa pongezi hizo kwa wanachama wa Umoja huo waliotembelea Ofisini kwake kwa lengo la kuelezea namna wanavyoshiriki katika kukuza Viwanda kupitia chama hicho cha Usindikaji wa Vyakula.
"Tafopa mnafanya kazi nzuri ambayo moja kwa inaisaidia Tanzania ya Viwanda; kuunganisha watu katika maeneo ya kuwapa elimu ya namna ya kusindika Vyakula kwa namna moja mnatoa ajira kwa watanzania na mnaongeza thamani ya mazao ambayo bila kusindikwa yangeweza kuharibika na kusabisha hasara kwa Wakulima" Alisema Jafo.
Serikali itaendelea kuwashirikisha katika fursa mbalimbali zinazoendelea kutokea na kuwakutanisha na wadau wa maendeleo ili muweze kuwa na Uhakika wa masoko, Mpate maeneo ya kujengea viwanda vya kusindika vyakula na kutatua changamoto zingine zinazowakabili, alimalizia Jafo.
Alizungumza katika kikao hicho Mwenyekiti ya TAFOPA Suzy Laiser amesema mpaka sasa hivi umoja huo una jumla ya wanachama zaidi ya 600 ambao wote wanajishighulisha na usindikaji vyakula na wamekua wakoshiriki na maonyesho ya Taifa ya biashara lakini bado wanakabiliwa na uhaba wa maeneo ya kujenga viwanda kwa ajili ya kazi hiyo.
Aliongeza kuwa wanaishkuru Shirika la Viwanda Vidogo Vidogo (Sido) kwa kuendelea kutoa mafunzo kwa Wanachama ambao wamepata ujuzi zaidi wa kusindika vyakula vya aina mbalimbali lakino changamoto ni ukosefu wa maeneo ya kufanyia kazi zao. Hivyo wengi hufanyia nyumbani ambapo hawawezi kupata Nembo ya Ubora kutoka Tbs nk.
Waziri Jafo alifunga kikao kwa kusema kuwa Suala la Maeneo liko katika Mamlaka za Serikali za Mitaa hivyo atawakutanisha wanachama hao na Viongozi wa Wilaya na Mkoa ili waweze kuangalia suala hilo kwa mapana yake.