Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo(katikati) akikagua ukamilishaji wa Hospital ya Wilaya ya Hai alipofanya ziara yake katika Wilaya Hiyo.
Hili ni kati ya majengo yanayoendelea kujengwa katika Hospital ya Wilaya ya Hai.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo akizuangumza na watumishi wa Idara ya Afya wakati alipotembelea Hospital ya Wilaya ya Hai.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Mkoa wa Kilimanjaro, Wilaya na Siha pamoja na watumishi wa Halmashauri hiyo.
.................................................................
Nteghenjwa Hosseah, Siha.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo amesema atafanya kila liwezekanalo kupata Fedha zaidi kwa ajili ya ukamilishaji ya hospital ya Wilaya ya Siha.
Waziri Jafo amesema hayo alipokua akifuatilia Agizo lake alilolitoa miezi kadhaa iliyopita ya kuacha kutumia Mkandarasi na kutumia Mafundi wa jamii "Force Account" katika ujenzi wa hospital hiyo ambapo Halmashauri ya Siha ilishatoa kazi hiyo kwa Mkandarasi na gharama za ujenzi kuwa juu zaidi.
"Katika ziara yangu iliyopita Kazi ilikua haijaanza na bado mlikua mnajadiliana na Mkandarasi mlinieleza kuwa zinahitajika Fedha zaidi kwa ajili ya kukamilisha kazi hii kwa mujibu wa Mkandarasi ndipo niliposhauri mtumie Mafundi wa kijamii "Force Account" na sio Mkandarasi kama mlivyopanga hapo awali" alisema Jafo.
Aliongeza "nimefurahi kuwa mlinielewa na mkazingatia ushauri wangu na leo hii ninaona matunda ya matumizi ya mafundi wa kijamii ambao wamefanya kazi nzuri kwa ubora wa hali ya juu na gharama nafuu katika hili hongereni sana".
Alisisitiza kuwa Nimeona majengo ambayo yanakaribia kukamilika lakin pia nimeskia taarifa yenu kuwa bado kuna majengo zaidi yanahitajika ila kukamilisha hadhi ya hospital ya Wilaya ninaahidi kuwatafutia Fedha kwa ajili ya Ukamilishaji wa majengo hayo.
Akisoma taara ya Afya Mganga Mkuu wa Wilaya hiyo Dr Andrew Method amesema Wilaya hiyo unakabiliwa na changamoto kubwa ya Uhaba wa Hospital ya Wilaya na vituo vya Afya vilivyopo ni vitano tu ambavyo kati ya hivyo cha Serikali ni kimoja tu hivyo nguvu kubwa imewekwa katika kuhakikisha wanapata miundombinu bora ya hospital ya Wilaya.
" Fedha tulizopata ilikua ni Mil 200 na kwa kuzingatia maelekezo yako tulitumia Force Account na kama unavyoona Mhe. Waziri kazi iko katika hatua za mwishoni na tumebada majengo mengi zaidi ya ramani ya awali".
Ujenzi wa Hospital hii utakapokamilika utawezesha Wilaya ya Siha kuwa hospital nmoja ya Wilaya pamoja na ile ya Kibong'oto iliyoko chini ya Wizara ya Afya.