Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Batilda Burian leo tarehe 17/01/2022 akitoa nasaha zake kwa Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mambali iliyopo Wilayani Nzega alipofanya ziara katika Shule hiyo ikiwa ni Siku ya kwanza tangu Shule ifunguliwe. Mhe. Mkuu wa Mkoa aliwasisitiza wanafunzi hao kusoma kwa bidii ili wafanye vizuri katika masoma yao na watokomeza daraja 0.
Kupitia Fedha za Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya UVIKO 19 Shule ya Sekondari Mambali imejenga madarasa manne yaliyogharimu kiasi cha Tsh. Milioni 80.