Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini B Hamid Seif Said amewataka watendaji wa Afya kufanya kazi kwa kuzingatia sheria na miongozo ya utumishi wa umma
Ili kutoa huduma bora kwa wananchi
Akizungumza
na watendaji hao ofisini kwake mahonda Katika kikao cha kuutambulisha
watendaji wapya wa sekta ya afya katika wilaya hiyo
Amesema
sekta ya afya ni sekta muhimu Kwa maendeleo ya jamii hivyo ipo haja Kwa
Kila mtumishi kuzingati sheria na miongozo iliyowekwa na serikali
Amewataka
watendaji hao kuwa na utaratibu wa kutembelea vituo vya afya Ili
kubaini matatizo yaliyopo na kuyatafutia ufumbuzi wa haraka pamoja na
kuhimiza uwajibikaji kwa watendaji wa vituo vya afya
Amefahamisha
kuwa kuna baadhi ya vituo vya afya mahudhurio yake hayaridhishi hivyo
ni vyema Kwa viongozi hao kusimamia ipasavyo Kwa kuhakikisha Kila
mtumishi anafika mapema katika kituo chale cha kazi
Hata
hivyo bwana Hamid amewataka watendaji hao kushughulikia matatizo ya
vituo vya Afya donge mtambile,kiomba mvua pamoja na kituo Cha afya
bumbwini makoba Kwa kuimarisha miundombinu ya vituo hivyo Ili viweze
kutoa huduma Kama inavyotakiwa
Kwa
upande wao watendaji hao wameahidi kushirikiana na ofisi ya mkuu wa
wilaya pamoja na kuomba kusaidiwa ofisi kwani Kwa Sasa ofisi
wanayoitumia ni ndogo na haikidhi mahitaji.