MKUU WA WILAYA YA LUSHOTO AONGOZA HARAMBEE YA KUCHANGIA UJENZI WA NYUMBA ZA POLISI WILAYA YA LUSHOTO
Mkuu
wa Wilaya ya Lushoto ndugu Kalisti Lazaro ameongoza Harambee ya
Kuchangia Ujenzi wa Nyumba za Askari wa Jeshi la Polisi Wilaya ya
Lushoto.
Mkuu wa Wilaya aliambatana na Mbunge wa Jimbo la Lushoto
Alhaji Shabani Omary Shekilindi, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya
Lushoto ndugu Mathew Mbaruku, Msaidizi wa Kamanda wa Jeshi la Polisi
Mkoa wa Tanga Kamanda David Mafwimbo na Kamanda wa Traffic Mkoa wa Tanga
Kamanda ...
Harambee hiyo ya Kuchangia Fedha za Ujenzi wa Nyumba
za Polisi Lushoto ilifanyika kwenye Ofisi za Jeshi la Polisi Wilaya ya
Lushoto na ilihudhuriwa na Wafanyabiashara mbalimbali wa Wilaya ya
Lushoto, Wakuu wa Taasisi za Umma na Binafsi na Taasisi za Dini zilizopo
katika Wilaya ya Lushoto.
Jumla ya Tsh 1,460,000/= zilitolewa
papo hapo na Ahadi ya Tsh 19,300,000/= ilitolewa huku Mchanga Lori 14 na
Mifuko 1,230 ya Cement ikihaidiwa kutolewa kufanya Jumla ya Tsh
20,760,000/= na Ahadi ya Mifuko ya Cement 1,230 na Lori 14 za Mchanga Akiwakaribisha
Wadau Mkuu wa Wilaya alisema "Karibuni sana katika Jambo hili jema,
ninajisikia faraja kuona mmeitikia wito wangu na wakati ninawaalika
sikuwaambia kuwa tunakuja kufanya Harambee ya Kuchangia Ujenzi wa Nyumba
za Askari. Tumewazungusha kwenye Jengo hili jipya ambalo ndiyo litakuwa
Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Lushoto ili mjionee wenyewe hali ilivyo
na tumewapeleka mkaone zile Nyumba za Askari wetu wanazoishi kwa sasa,
kwa kweli hazina hadhi na hazifai kabisa kuwa Makazi ya watu. Serikali
Kuu imetoa Tsh 250,000,000/= kumalizia Jengo la Makao Makuu ya Jeshi la
Polisi Lushoto na tayari Jeshi la Polisi limeshatoa Tsh 167,000,000/=
kwa ajili ya Ujenzi wa Nyumba za Askari wa Jeshi la Polisi Wilaya ya
Lushoto. Nimeona niwaite ili tuongeze nguvu kuikamilisha kazi hii kwa
wakati. Makadirio ya Ujenzi wa Nyumba za Askari wa Jeshi la Polisi
Lushoto ni Tsh 300,000,000/=
Naye Kamanda David Mafwimbo ambaye
ni Msaidizi wa Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Tanga aliwapongeza
Wadau kwa Kuhudhuria na namna walivyolipokea Jambo hilo kama la kwao na
Kuchangia Fedha na Vifaa, Kamanda David Mafwimbo alisema, " Kwanza pok
|