Comoro kushirikiana na Tanzania katika sekta za kimkakati asema Rais Azali Anena
Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Visiwa vya Comoro Mheshimiwa Saidi Yakubu amekutana na kufanya mazumgumzo na Rai...
BALOZI KOMBO AKUTANA NA WADAU WA NGO’s JIJINI ROMA
Written By CCMdijitali on Monday, February 28, 2022 | February 28, 2022
Balozi wa Tanzania nchini Italia Mh. Mahmoud Thabit Kombo akipokea zawadi ya kitabu kutoka kwa mmoja wa wadau wa NGO's mwishoni mwa wiki Jijini Roma, Italia |
Balozi wa Tanzania nchini Italia Mhe. Mahmoud Thabit Kombo akipokea akiwa katika kikao na wadau wa NGO's mwishoni mwa wiki Jijini Roma, Italia |
Na Mwandishi wetu, Roma
Balozi wa Tanzania nchini Italia Mhe. Mahmoud Thabit Kombo amekutana na kufanya mkutano na wadau wa NGO’s takribani sitini na nne zinazofanya shughuli zake nchini Tanzania mwishoni mwa wiki Jijini Roma, Italia.
Mkutano huo ulihudhuriwa pia na wadau mbalimbali wa Diaspora pamoja na wadau wa NGO walimpongeza Mhe. Balozi kwa kuwapa nafasi ya kujitambulisha na kutoa fursa ya kuwasikiliza mafanikio yao sambamba na changamoto wanazopitia katika kufanikisha shughulika zao nchini Tanzania.
Pamoja na kuwasikiliza lakini pia Balozi alitumia nafasi hiyo kuwashauri kuwa na ushirikiano wa pamoja ili kuleta ufanisi zaidi kwenye maeneo wanayo yafanyia kazi. Aidha, katika mkutano huo Balozi Kombo aliongea mubashara na Balozi wa Italia nchini Tanzania Mhe. Marco Lombardi na kumpa fursa ya kutoa salaam zake moja kwa moja kwa njia ya mtandao.
Balozi wa Italia nchini Tanzania aliwahakikishia wadau hao kuwa wapo kwenye mikono salama ya Balozi wa Tanzania Rome na chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kuwa Tanzania ni nchi salama ya kufanya shughuli zao.
KATIBU MKKU WIZARA YA AFYA ATOA MAAGIZO MKOANI SINGIDA
Written By CCMdijitali on Sunday, February 27, 2022 | February 27, 2022
RAIS SAMIA AKUTANA NA MTENDAJI MKKU WA AIRTEL AFRIKA