MBUNGE wa Nanyamba(CCM),Abdallah Chikota |
CHIKOTA AIOMBA SERIKALI ITOE KIBALI MAALUM CHA AJIRA ZA WALIMU NA AFYA
MBUNGE
wa Nanyamba(CCM),Abdallah Chikota ameiomba serikali kutoa kibali maalum
cha kuajiri walimu na watumishi wa kada ya afya kutokana na kuwepo kwa
uhaba mkubwa wa watumishi hao nchini.
Chikota amesema hayo bungeni alipokuwa akichangia taarifa ya Kamati ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii.
Amesema
kutokana na hali ilivyo kwenye Halmashauri baada ya kujengwa
miundombinu ya madarasa na vituo vya afya ni vyema serikali ikachukua
hatua za makusudi kuajiri watumishi wa sekta hizo.
“Kazi kubwa ambayo imefanywa na Rais Samia Suluhu Hassan ya ujenzi wa madarasa 15,000, vituo vya afya, faida za ujenzi wa miundombinu hii haitaonekana kama upungufu huu ukiendelea naomba serikali ichukue hatua za makusudi kutoa kibali maalum kwa ajili ya kuajiri walimu na watumishi wa sekta ya afya.”
“Naiomba serikali yangu sikivu itoe kibali maalum kama ilivyofanya miaka ya nyuma tulivyokuwa na uhaba wa wahasibu,”amesema.