Mhe.Kassim Majaliwa Majaliwa ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania |
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa ameridhia kuongeza muda wa siku saba kwa kamati
maalum iliyopewa jukumu la kuchunguza mauaji yaliyofanyika Mtwara na
Kilindi, Tanga.
Kamati hiyo
iliyoanza kazi Februari 4, 2022 ilipaswa kukamilisha ripoti yake ndani
ya siku 14, zilizoishia Februari 17, 2022. Lakini kutokana na ukubwa wa
kazi na mahitaji ya kujiridhisha na baadhi ya masuala, kamati imeomba
kuongezewa siku saba kuanzia Februari 17 hadi Februari 23, 2022.
Kamati
hiyo iliundwa na Waziri Mkuu ikiwa ni utekelezaji wa agizo la
Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan alilolitoa Februari 4, 2022 mjini
Magu, Mwanza akiwa njiani kuelekea Musoma, Mara kwenye maadhimisho ya
miaka 45 ya CCM.
Aidha,
Mheshimiwa Waziri Mkuu anatoa wito kwa mamlaka husika kuendelea kutoa
ushirikiano kwa kamati ili iweze kuikamilisha kazi hiyo kwa wakati na
ufanisi