UKAGUZI WA BARABARA JIMBONI
Mbunge
wa Jimbo la Igunga Mhe. Nicholaus Ngassa ameanza ziara ya siku tano ya
kukagua maendeleo ya ujenzi wa Barabara za Mitaa na Vitongoji.
Mheshimiwa
Mbunge akiwa ameambatana na Mheshimiwa Diwani wa Kata ya Igunga, Mtendaji
wa Kata, Mwenyekiti wa Kitongoji cha Kati na Mhandisi wa TARURA Wilaya
wametumia ziara hii mahususi kutembelea Barabara zilizoharibiwa na Mvua
zinazoendelea kunyeesha kwa ajili ya kuzipatia ufumbuzi.
Nukuu
".... Rais wetu Mhe. Samia Suluhu Hassan alipofanya uamuzi wa Fedha za Barabara kuletwa moja kwa moja kwa kila Jimbo, dhamira yake ilikuwa ni kuhakikisha ufanisi na usawa katika kutekeleza miradi ya Barabara. TARURA simamieni hii miradi, msilale kuhakikisha hizi Fedha zinatoa matokeo yanayoonekana kwa Wananchi, Barabara zijengwe kwa ubora na thamani ya Fedha ionekane kwa wana Igunga. Haitapendeza tujenge Barabara za Lami alafu mvua mbili tatu tuu zikinyeesha tunaanza kuona matobo juu ya Barabara..."
Nicholaus George Ngassa (Mb)
"Kazi na Maendeleo"
Imetolewa na:
Katibu wa Mbunge
Jimbo la Igunga