Jimbo la Igunga
"Tunaanzia Tulipoishia"
Mbunge wa Jimbo la Igunga Mhe. Nicholaus George Ngassa anatarajia kuanza ziara ya kutembelea miundombinu ya Barabara za Mitaa na Vitongoji.
Ziara ya Mheshimiwa Mbunge itaanza tarehe 21 Februari 2022 kwa ajili ya kukagua na kuona maendeleo ya ujenzi wa Barabara zinazojengwa kwa kiwango cha lami, barabara zinazojengwa kwa changarawe na moramu kwenye Mitaa na Vitongoji vya Jimbo la Igunga.
Aidha Mheshimiwa Mbunge ataambatana na Wahandisi wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA), Mheshimiwa Diwani na Wenyeviti wa Mitaa na Vitongoji kukagua Barabara za Mitaa na Vitongoji zilizoharibiwa na Mvua za masika zinazoendelea kunyeesha kwa ajili ya kuzipatia ufumbuzi.
"Kazi na Maendeleo"
Imetolewa na:
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Igunga