MHE. ZUNGU ACHAGULIWA KUWA NAIBU SPIKA
Mbunge wa Ilala, Mhe.
Mussa Azan Zungu amechaguliwa kuwa Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kwa kura 296 kati ya kura 301 zilizopigwa na
Waheshimiwa Wabunge walikuwepo Bungeni.
Mara baada ya kuchaguliwa Mhe. Zungu aliapishwa na Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson Bungeni Jijini Dodoma.
Akizungumza
mara baada ya kuapishwa Mhe. Zungu aliwashukuru Waheshimiwa Wabunge na
Chama chake cha Mapinduzi kikiongozwa na Mwenyekiti wake, Mhe. Samia
Suluhu Hassan kwa kumpendekeza na hatimaye kuchaguliwa kushika nafasi
hiyo.
Aidha, Mhe. Zungu ameahidi kushirikiana na Waheshimiwa Wabunge kwa kufanya kazi kwa bidii ili kujenga Taifa.