Home » » MRADI WA MAJI SAFI NA SALAMA WA MUGANGO,KIABAKARI, BUTIAMA MKOANI MARA WAWEKWA JIWE LA MSINGI

MRADI WA MAJI SAFI NA SALAMA WA MUGANGO,KIABAKARI, BUTIAMA MKOANI MARA WAWEKWA JIWE LA MSINGI

Written By CCMdijitali on Sunday, February 6, 2022 | February 06, 2022

Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, aweka jiwe la msingi mradi wa Maji safi na Salama wa Mugango, Kiabakari, Butiama Mkoani Mara.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Viongozi wa Chama cha Mapinduzi CCM wa Mkoa Mara alipowasili katika Kijiji cha Mugango Wilaya ya Musoma Vijijini kwa ajili ya kuweka jiwe la Msingi Mradi wa Maji Safi wa Mugango,Kiabakari,Butiama leo tarehe 06 Februari, 2022.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiondoa Kitambaa kama ishara kuweka jiwe la Msingi Mradi wa Maji Safi wa Mugango,Kiabakari,Butiama katika Kijiji cha Mugango Wilaya ya Musoma Vijijini Mkoani Mara  leo tarehe 06 Februari, 2022.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Wananchi wa Kijiji cha Mugango Wilaya ya Musoma Vijijini Mkoani Mara Baada ya kuweka jiwe la Msingi Mradi wa Maji Safi wa Mugango,Kiabakari,Butiama leo tarehe 06 Februari, 2022, Mhe. Rais Samia yupo katika ziara ya Kikazi ya siku nne Mkoani Mara kutembelea kukagua Miradi mbalimbali ya maendeleo ya Wananchi.

Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Awesu akicheza ngoma ya Singeli pamoja na Viongozi mbalimbali na Wananchi wa Kijiji cha Mugango Wilaya ya Musoma Vijijini Mkoani Mara mara Baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, kuweka jiwe la Msingi Mradi wa Maji Safi wa Mugango,Kiabakari,Butiama leo tarehe 06 Februari, 2022, Mhe. Rais Samia yupo Mkoani Mara kwa ziara ya kikazi ya siku nne ya kutembelea kukagua Miradi mbalimbali ya maendeleo ya Wananchi.


Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link