Home » » MSITU WA KIWENGWA - ZANZIBAR

MSITU WA KIWENGWA - ZANZIBAR

Written By CCMdijitali on Monday, February 7, 2022 | February 07, 2022

Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini B Mhe Hamid Seif Said

 Wilaya ya Kaskazini B

Mkuu wa wilaya ya Kaskazini B Mhe Hamid Seif Said Amesema atashirikiana na idara ya misitu kwa ajili ya kuoneshana mipaka halisi ya hifadhi ya msitu wa kiwengwa na kumaliza mgogoro na wananchi wanaoishi karibu na msitu huo.


Amesema wapo baadhi ya wananchi wamekuwa wakilalamika kuwa kuna baadhi ya watu wamejitokeza hivi karibuni na kuweka alama za mipaka katika eneo lao ambalo wamekuwa wakilitumia Kwa shughuli za kilimo Kwa muda mrefu.


Akizungumza na wananchi mbalimbali katika eneo la hifadhi ya msitu huko kiwengwa kairo Amesema taarifa aliyonayo ni kwamba katika eneo Hilo vipo viwanja vilivyokatwa mwaka 2008 Kwa ajili ya Ujenzi wa ofisi mbalimbali za vyombo vya ulinzi na usalama.

 
Hivyo amewataka wananchi kuwa wastaamilivu wakati uongozi wa wilaya unakusudia kuwaita watendaji wa idara ya misitu Ili kuweka wazi mipaka ya hifadhi hiyo.


Hata hivyo bwana Hamid amewataka wananchi hao kufuata taratibu za serikali pindi wanapotaka kuyatumia maeneo ya wazi yaliyomo karibu na makaazi yao Ili kuepusha mgogoro pindi serikali inapotaka kuyatumia Kwa ajili ya shughuli za maendeleo.


Nao baadhi ya wananchi wamemueleza mkuu huyo wa wilaya kuwa hifadhi ya msitu wa kiwengwa umekuwa ukibadilishwa mipaka mara Kwa mara na kusabisha baadhi ya wananchi kuonekana kuwa wamo ndani ya hifadhi ya msitu huo
 
Hata hivyo wananchi hao wamesema licha ya kuzuiwa kutumia eneo la hifadhi Kwa Ujenzi wa nyumba pamoja na kilimo lakini wapo baadhi ya wananchi kutoka nje ya kiwengwa ambao wamekuwa na vielelezo vinavyoonesha kuwa na viwanja katika hifadhi hiyo.

Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link