Home » , » RC BALOZI BATILDA AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MKURUGENZI MKUU WA KAMPUNI YA JTI

RC BALOZI BATILDA AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MKURUGENZI MKUU WA KAMPUNI YA JTI

Written By CCMdijitali on Thursday, February 10, 2022 | February 10, 2022

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Batilda Burian (kushoto) akiongea na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya JTI Bw. Sarel Bicaci.

 

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Batilda Burian leo tarehe 10 Februari, 2022 Ofisini kwake amekutana na kuzungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya JTI Bw. Sarel Bicaci. Mazungumzo hayo yalijikita namna Kampuni ya Ununuzi wa tumbaku ya JTI itakavyotoa mchango wake utakaoboresha utoaji wa huduma za Afya na Elimu Mkoani Tabora, ambapo katika mwaka huu wa Fedha Kampuni ya JTI imetenga kiasi cha Tsh Milioni 690 itakayotumika kukamilisha ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Wilayani Urambo. Ujenzi unatarajia kuanza mwezi huu wa Februari. Pia Kampuni hiyo imechangia Viti 700 na meza 700 kwa ajili ya Shule za Sekondari za Wilaya ya Uyui, Urambo na Kaliua.

Katika Sekta ya Afya kwa Mwaka huu wa Fedha imetenga kiasi cha Tsh Milioni 180 kwa ajili ya ukamilishaji wa ujenzi wa zahanati katika Kijiji cha Ipululu Wilayani Uyui.

Pia Kampuni ya JTI imetenga Fedha kiasi cha Tsh. Milioni 150 kwa ajili ya kuchimba Malambo 6 Wilayani Kaliua yatakayotumika kumwagilia vitalu vya miti, bustani za mboga za majani na mabedi ya tumbaku.

Aidha, Katika Sekta ya Ufugaji Nyuki Kampuni hiyo imetenga Tsh. Milioni 22 kwa ajili ya utengenezaji wa mizinga ya nyuki kwa vikundi vya ufugaji nyuki vya Wilaya za Uyui, Kaliua na Urambo.

Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link