SERIKALI YAFUNGULIA MAGAZETI YALIYOFUNGIWA
|
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknollojia ya Habari, Nape
Nnauye akikabidhi leseni ya magazeti yaliyofungiwa ya Mseto na Mwanahalisi kwa
Said Kubenea baada ya magazeti hayo kufungiwa kwa zaidi ya miaka miwili.
Makabidhiano hayo yamefanyika kwenye ukumbi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania,
Dar es Salaam. Anayeshuhudia kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Jim
Yonazi na kulia ni Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Deodatus Balile |
|
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknollojia ya Habari, Nape
Nnauye akikabidhi leseni ya gazeti lililofungiwa la Mawio kwa Erasto Massawe
baada ya magazeti hayo kufungiwa kwa zaidi ya miaka miwili. Makabidhiano hayo
yamefanyika kwenye ukumbi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, Dar es Salaam.
Anayeshuhudia kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Jim Yonazi na kulia
ni Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Deodatus Balile
|
|
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape
Nnauye akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari (hawapo pichani) kabla ya
kukabidhi leseni ya magazeti yaliyofungiwa ya Mseto, Mwanahalisi, Mawio na
Tanzania Daima kwenye ukumbi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, Dar es Salaam
|
|
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia
ya Habari, Dkt. Jim Yonazi akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari kabla
ya Waziri wa Wizara hiyo, Nape Nnauye kufungulia magazeti ya Mawio,
Mwanahalisi, Mseto na Tanzania Daima yaliyofungiwa zaidi ya miaka miwili kwenye
kikao na wahariri hao pichani kilichofanyika kwenye ukumbi wa Mamlaka ya
Mawasiliano Tanzania, Dar es Salaam
|
|
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape
Nnauye akiteta jambo na kufurahi na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Jim Yonazi
wakati wa kikao chake na wahariri wa vyombo vya habari kilichofanyika kwenye
ukumbi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, Dar es Salaam baada ya kufungulia
magazeti ya Mawio, Mwanahalisi, Tanzania Daima na Mseto
|
|
Wahariri wa vyombo vya habari wakimsikiliza kwa makini
Waziri wa Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye (hayupo
pichani) wakati wa kikao chake na wahariri hao kilichofanyika kwenye ukumbi wa
mikutano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, Dar es Salaam ambapo alifungulia
magazeti ya Mseto, Mawio, Mwanahalisi na Tanzania Daima yaliyofungiwa zaidi ya
miaka miwili.
|
|
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape
Nnauye (wa saba kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na wahariri wa vyombo vya
habari baada ya kikao chake na wahariri hao kilichofanyika kwenye ukumbi wa
mikutano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, Dar es Salaam. Wa sita kulia ni
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Jim Yonazi
|
|
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape
Nnauye akizungumza na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Jim Yonazi baada ya
kufungulia magazeti ya Mawio, Mwanahalisi, Tanzania Daima na Mseto kwenye kikao
chake na wahariri kilichofanyika ukumbi wa mikutano wa Mamlaka ya Mawasiliano
Tanzania, Dar es Salaam. Wa kwanza kulia ni Naibu Katibu wa Wizara hiyo,
Mohammed Khamis na kushoto ni Gerson Msigwa, Mkurugenzi wa Idara ya Habari –
MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali.
|