Home » » Waziri Dkt Gwajima atoa taarifa ya mafanikio na changamoto za Mashirika yasiyo ya Kiserikali nchini

Waziri Dkt Gwajima atoa taarifa ya mafanikio na changamoto za Mashirika yasiyo ya Kiserikali nchini

Written By CCMdijitali on Sunday, February 6, 2022 | February 06, 2022

 

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima
 

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima amebainisha kuwa, jumla ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali 6,147 ndiyo yanatekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria na kanuni kati ya Mashirika 11,946 yaliyosajiliwa mwaka 2005 hadi Januari, 2022.


Mhe.Dkt. Gwajima amebainisha hayo wakati akitoa taarifa ya usimamizi, utekelezaji, mafanikio na changamoto za Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini kwa kipindi cha 2019/2021 mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Maendeleo ya Jamii jijini Dodoma.


Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Huduma za Maendeleo ya Jamii Mhe. Aloyce Kamamba, amesema hakuna sababu ya kuwa na orodha kubwa ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali wakati yanayofanya kazi kwa mujibu wa sheria ni Mashirika machache.


Baadhi ya wajumbe wa Kamati hiyo wamepongeza jitihada zinazofanywa na Wizara katika kufuatilia na kusimamia utekelezaji wa NGOs na kusisitiza kuboresha mikakati iliyopo.






Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link