WAZIRI WA AFYA ZANZIBAR APOKEA MASHINE ZA OXYGEN ZENYE THAMANI YA TSH MILION 14 KUTOKA KWA DORIS MOLLEL FOUNDATION KWA KUSHIRIKIANA NA SEGALFOUNDATION
Waziri wa Afya Zanzibar Apokea Mashine za Oxygen.
Waziri
wa Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto Zanzibar Mhe. Nassor
Ahmed Mazrui amepokea mashine tatu za kufua oxygen zenye thamani ya Tsh.
Millioni 14 kutoka kwa @dorismollelfoundation kwa kushirikiana na
@segalfoundation mashine hizi ni kwa ajili ya kusaidia vitengi vya
watoto njiti katika Hospitali ya Fuoni iliyoko Magharibi B, Unguja,
Zanzibar
Vifaa hivi
vilipokelewa katika hafla fupi iliyofanyika katika Hospitali ya Fuoni na
kuhudhuriwa na Viongozi kutoka Wizara ya Afya, Ofisi ya Mrajis wa
Mashirika yasiyo ya kiserikali, viongozi kutoka @segalfoundation
wakiongozwa na Mkurugenzi wa Programs Bi. Gladys Onyango pamoja na wadau
wa Afya, Zanzibar.