KAMATI YA BUNGE YA LAAC YAKAGUA
UKARABATI WA SHULE KONGWE YA
SEKONDARI RUNGWE
Kamati
ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) imekagua mradi
wa ukarabati wa Shule ya Sekondari Rungwe na kupongeza namna Shule
hiyo ilivyokarabatiwa.
Akizungumza na Watendaji wa Halmashauri ya
Rungwe iliyopo Mkoani Mbeya mara baada ya kukagua ukarabati huo Kaimu
Mwenyekiti Kamati ya LAAC, Mhe. Boniphace Butondo amesema wameridhika
kwa namna ukarabati wa Shule hiyo kongwe ulivyofanywa.
Aidha
Mhe. Butondo amewataka Watendaji wa Halmashauri hiyo kufanyia kazi
mapungufu machache yaliyobainika ikiwemo uhaba wa vyoo na bafu katika
baadhi ya mabweni.
Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe ilipokea
milioni 752 kwa ajili ya ukarabati huo ambapo fedha hizo zimetumika
kukarabati vyumba 38 pamoja na ujenzi wa mabweni mawili, ujenzi wa
vyumba vitatu vya madarasa na ujenzi wa ofisi moja.