Home » » KAMATI YA BUNGE YAIPONGEZA WIZARA YA ARDHI - SINGIDA

KAMATI YA BUNGE YAIPONGEZA WIZARA YA ARDHI - SINGIDA

Written By CCMdijitali on Wednesday, March 16, 2022 | March 16, 2022

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi Maliasili na Utalii Ally Makoa akizungumza na wananchi wa vijiji vya Ntondo na Nkwea vilivyopo halmashauri ya wilaya ya Singida mkoani Singida wakati kamati hiyo ilipokwenda kukagua mradi wa mipango ya matumizi ya ardhi katika vijiji hivyo tarehe 15 Machi 2022.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza na wananchi wa vijiji vya Ntondo na Nkwea mkoani Singida wakati kamati ya Bunge ya Ardhi Maliasili na Utalii ilipokwenda kukagua mradi wa mipango ya matumizi ya ardhi katika vijiji hivyo tarehe 15 Machi 2022.

 
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akiwa katika picha ya pamoja na wananchi wa vijiji vya Ntondo na Nkwea mkoani Singida baada ya kukabidhiwa hatimiliki za kimila wakati wa ziara ya kamati ya Bunge ya Ardhi Maliasili na Utalii katika hivyo tarehe 15 Machi 2022.

Mbunge wa Viti Maalum Babati mkoani Manyara Asia Abdulkarim Halamga akitoa hati kwa mkazi wa kijiji cha Ntondo mkoani Singida Benjamin Shija wakati kamati ya Bunge ya Ardhi Maliasili na Utalii ilipokwenda kukagua mradi wa mipango ya matumizi ya ardhi katika vijiji hivyo tarehe 15 Machi 2022.

 

KAMATI YA BUNGE YAIPONGEZA WIZARA YA ARDHI

 

Na Munir Shemweta, WANMM SINGIDA


Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kufanikisha kuandaliwa Mpango wa Matumizi ya Ardhi pamoja na upimaji ardhi kwenye vijiji vya Ntondo na Nkwea vilivyopo halmashauri ya wilaya ya Singida katika mkoa wa Singida.


Aidha, Kamati hiyo imempongeza pia Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuridhia kutolewa shilingi Bilioni 50 kwa ajili ya mradi wa kupanga, kupima na kumilikisha ardhi unaotekelezwa katika halmashauri nchini.

 

Halmashauri ya wilaya ya Singida ina jumla ya vijiji 84 kati ya vijiji hivyo vijiji 20 vinapitiwa na Mkuza wa Bomba la Mafuta na Mipango ya Matumizi bora ya ardhi imeandaliwa katika vijiji 16 kati ya 20 na kufanya jumla ya vijiji 50 katika wilaya ya Singisa kuwa na mipango ya matumizi bora ya ardhi.


Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi Maliasili na Utalii imeitaka Wizara ya Ardhi kuongeza kasi ya upangaji, upimaji na umilikishajj ardhi kwenye maeneo mbalimbali ili kufikia mwaka 2025 iwe imetimiza malengo na matakwa ya Wizara na kuboresha sekta ya ardhi ili kuiwezesha serikali kuinua uchumi.

Akizungumza wakati wa ziara ya Kamati ya Bunge katika vijjiji vya Ntondo na Nkwea tarehe 15 Machi 2022 Mwenyekiti wa Kamati  hiyo Ally Makoa alisema, kazi ya upangaji na upimaji iliyofanywa na wizara ya ardhi kupitia mradi wa KKK unatimiza kiu na matarajio ya Wizara pamoja na ilani ya Chama cha Mapinduzi.


"Tunamshukuru Mhe. Rais Samia kwa kuridhia shilingi Bilioni 50 kuja katika mpango wa kupanga kupima na kumilikisha ardhi, tunaishukuru Wizara ya Ardhi kwa kujituma na kuandaa hati. Fedha zilizotolewa na serikali kupitia Wizara ya Fedha zinajibu matarajio ya ilani ya ccm" alisema Makoa


Kwa mujibu wa Makoa, kamati yake inatamani maeneo yote yaliyozingatiwa kwenye mipango ya upangaji na upimaji yanazingatiwa kwa kuwekewa alama zinazoonesha mipaka na matumizi ya maeneo ili kuepuka uvamizi unaoweza kufanywa na baadhi ya watu.


"Kamati inatamani upimaji unazingatiwa ili kutumiza malengo yote yaliyoaninshsa ili asitokee mtu kutoka eneo A kwenda B hivyo lazima kuwepo vibao kuonesha eneo maana leo wanakuja wavamizj kuvamia enso kw kuwa hajuna alama"" alisema Makoa.

 

Mbunge wa Viti Maalum Babati mkoani Manyara Asia Abdulkarim Halamga alisifu juhudi zinazofanywa na Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi katika utekelezaji wa mipango yake katka masuala ya matumizi bora pamoja na upimaji ardhi.

‘’Napenda niipongeze wizara ya ardhi pampja na wafanayakazi wake wote kwa kazi kubwa wanaiyoifanya katika kutekeleza majukumu yake ikiewemo upimaji ardhi kwenye maeneo mbalimbali hii itasaidia sana kuondokana na migogoro ya ardhi ambayo mingi husababishwa na kutopimwa kwa maeneo’’ alisema Asia.

Akizungumza mbele ya Kamati hiyo, Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula alieleza kuwa, uandaaji mipango ya matumizi ya ardhi hupitia hatua mbalimbali ili kuwezesha usalama wa milki, utunzaji wa mazingira na kuongeza tija katika shughuli za kiuchumi.

Kwa mujibu wa Dkt Mabula, hatua nyingine ni pamoja ni kuandaa mipango kina na usimamizi wake pamoja na utoaji hati miliki za kimila na utawala wa ardhi.

‘’Wizara yangu imeendelea kuongeza kasi katika kuhakikisha inapanga, kupima na kumilikisha maeneo mengi nchini ili kupunguza ama kuondoa migogoro ya ardhi na tumshukuru mhe Rais Samia kwa kutuwezesha kutupatia fedha za kuendesha miradi ya mbalimbali ya upimaji’’ alisema Dkt Mabula.

 

Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link