📍OPERESHENI ANWANI ZA MAKAZI
SASA NI ASILIMIA 67📍
Operesheni
ya uwekaji wa Anwani za Makazi nchini iliyotangazwa tarehe 8 Februari
mwaka huu wa 2022 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia
Suluhu Hassan sasa utekelezaji wake umefikia asilimia 67 kulingana na
takwimu za mfumo unaopokea taarifa za utekelezaji wa Wizara ya Habari,
Mawasiliano na Teknolojia ya Habari
Taarifa hiyo imetolewa na
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye
wakati wa mkutano na Wakuu wa Mikoa yote nchini uliofanyika jijini
Dodoma uliolenga kutoa taarifa ya utekelezaji wa operesheni hiyo
“Tathimini iliyofanyika ya kupata asilimia 67 imezingatia kazi zilizotekelezwa ikiwa ni kazi ya kutambua maeneo; kujenga uwezo kwa maafisa na watendaji wanaofanya kazi hii; kutoa elimu ya zoezi husika; kukusanya taarifa; kutengeneza mfumo utakaopokea taarifa na kuingiza taarifa kwenye mfumo ili ziweze kutumika na kuweka muundombinu (physical) katika maeneo mbalimbali nchini”, amezungumza Mhe. Nape
Ameongeza kuwa mwenendo wa utekelezaji unaonesha matumaini ya zoezi kukamilika kabla ya muda uliopangwa na kazi itakayofuata itakuwa ni kusafisha baadhi ya taarifa kwenye mfumo kwa hatua za kuukabidhi mfumo kwa mujibu wa maelekezo ya kuukabidhi ifikapo tarehe 22 Mei, mwaka 2022.
@samia_suluhu_hassan @ikulu_mawasiliano @ikulu_habari @kassim_m_majaliwa @napennauye @innocentbash @drjimyonazi @ortamisemi @wizara_ya_ardhi @tcra_tanzania @ucsaftz @ttcl_corporation @posta_tz