Home » , » SERIKALI YA AWAMU YA SITA IMEFANIKIWA KUSAJILI MIRADI 294 - WAZIRI KIJAJI

SERIKALI YA AWAMU YA SITA IMEFANIKIWA KUSAJILI MIRADI 294 - WAZIRI KIJAJI

Written By CCMdijitali on Friday, March 11, 2022 | March 11, 2022

Waziri wa Uwekezaji Viwanda na Biashara, Dk Ashatu Kijaji
 


Waziri wa Uwekezaji Viwanda na Biashara, Dk Ashatu Kijaji amesema Serikali  ya Awamu ya Sita imefanikiwa kusajili miradi ya uwekezaji 294 yenye thamani ya dola za marekani bilioni  8,129.3 ambazo ni sawa na Shilingi trillion 18.75 inayotoa ajira takribani 62,301 kuanzia Machi, 2021 hadi  Februari, 2022 ikilinganishwa na  2020/2021 ambao ulikuwa ni dola za kimarekani billion 1 tu.


Akiongea  Machi 10, 2022 Jijini Dar es Salaam katika mkutano na waandishi wa habari uliohusu mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita kwa kipindi cha mwaka mmoja madarakani, Dkt Kijaji amesema hati za makubaliano 37 zenye  thamani ya dola za marekani bilioni 8, ambazo ni sawa na Shilingi 18.5 trilioni zinazotarajiwa kuzalisha ajira takriban 214,575 zilisainiwa wakati wa Maonesho ya Expo 2020 Dubai.

Aidha  Dkt Kijaji alitaja Mafanikio mengine kuwa ni pamoja na uanzishaji wa  Kongano za Viwanda kwa lengo la kuwasaidia wakulima wadogo na wawekezaji wa ndani. Kongamano hizo ni pamoja na  ujenzi wa Kongano ya Viwanda vya Mafuta ya Kula mkoani Singida yenye ukubwa wa  ekari 45,000, Kongano la Sukari (Sugar Park) katika eneo la Dakawa na Kongano ya Viwanda Kwala Pwani yenye ukubwa wa ekari 2,500.

Mafanikio makubwa mengine ni Ujenzi Kongano za Viwanda vya Elsewedy Kigamboni lenye ukubwa wa Mita za Mraba milioni 2.2 ambapo uwekezaji wake unakadiriwa kuwa na thamani ya Dola za Marekani milioni 400. Takriban viwanda 100 na ajira za moja kwa moja 50,000 zitazalishwa katika kongani hii ya viwanda Kigamboni.  Alisema Dkt. Kijaji.

Ili Kukabiliana na uhaba wa mbolea na kupitia makongamano ya Biashara na Uwekezaji Serikali imewezesha kupatikana kwa mwekezaji wa Kiwanda cha Mbolea kinachoitwa ITRACOM Fertilizer Tanzania Limited kitakachowekeza mtaji wa kiwanda hicho Dola za Kimarekani milioni 180 na kitaajiri wafanyakazi wa kudumu takriban 3000 na kitakuwa na uwezo uliosimikwa wa kuzalisha mbolea tani 500,000 kwa mwaka.

Aidha, Serikali imeendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji na ufanyaji biashara kwa kuunganisha na kufungamanisha mifumo ya kielektroniki ya utoaji wa vibali vya kazi kwa wageni na Upatikanaji wa Ardhi ya Uwekezaji pamoja na kutengeneza  mfumo wa pamoja wa kurahisisha uwekezaji

Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link