Wadau wa michezo wammwagia sifa Rais Samia
katika Mwaka mmoja
Watoa
mada mbalimbali kwenye kongamano la kuelezaea mafanikio ya michezo
lillilofanyika leo Machi 29, 2022 Dar es Salaam, wametoa shuhuda na
kupongeza mageuzi na mapinduzi makubwa huku wakisema mama Samia
ameupiga mwingi na kuondoka nao.
Aliyeanza ni Katibu Mkuu. Dkt,
Hassan Abbasi ambaye amesema Mhe. Rais amekuwa na utashi wa kisiasa
kwenye michezo, amefanya uwekezaji mkubwa na kuboresha na kujenga
miundombinu za michezo.
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu kwa
watu wenye Ulemavu (TAFF) Peter Sarungi amefafanua kuwa kutokana na
maono makubwa ya Mhe. Rais timu yao imefuzu kwenda kombe la dunia.
Aidha, ameongeza kuwa kutokana na utashi huo Mhe. Rais amefungua ajira kubwa za kitaifa na kimataifa kwa wachezaji walemavu.
Amesema hadi sasa wachezaji wanne (4) wameshapata timu katika mataifa mbalimbali duniani.
Kaimu
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Riadha Jackson Ndaweka amesema
mashindano ya taifa ya riadha yameweza kufanyika kwa mafanikio makubwa.
"Tunashukuru sana mama sasa tumeanza kupata udhamini kwa mashindano yetu kutoka katika mashirika ya Serikali" @mmchengerwa @dktabbasi @michuzijr @cloudsfmtz @nationalsportscouncil_bmt @tbc_online @habarileo_tz @dodoma_tv @dodoma_zone_ @wasafifm @efmtanzania @mwananchi_official @timesfmtz @swahilitimes @uhondotv