Wizara Hii ni Mali ya Watanzania - Gekul
Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Pauline Gekul @officialpaulinegekul
Machi 29, 2022 akiwa katika ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Chama cha
Waigizaji wa Filamu Tanzania Jijini Arusha amesema kuwa wizara ni mali
ya Watanzania na watendaji wake wanapaswa kufanya kazi kwa kuwasaidia
Watanzania wote bila ya ubaguzi.
“Hilo ninatoa ahadi kwenu kama kuna jambo ambalo limekwamishwa litakamilika mara moja na ninatoa siku saba likamike, kwani watendaji wote wizarani na kwenye taasisis zetu wanapaswa kushirikiana na wadau wote ambao ni nyinyi, hiyo ndiyo azma yangu na Waziri wangu mheshimiwa Mohamed Mchengerwa.”
Naibu Waziri Gekul aliwapongeza waigizaji wa filamu nchini Kwa kuendelea kufanya kazi kwa umoja, upendo na kujitokeza katika mikutano yote ya chama kwa wingi kwani serikali tangu wakati wa kupambana na Nduli Iddi Amin wasanii walishiriki vizuri, na hata wakati wa kupambana na janga la UVIKO 19 wasanii wamefanya kazi kubwa sana kuielimisha jamii ya Watanzania.
Kuhusu Ombi la waigizaji hao kumualika Rais Samia kushiriki kongamano kubwa la waigizaji nchini Naibu Waziri Gekul amesema atalifikisha na ana uhakika Mheshimiwa Rais atakubali.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Waigizaji Tanzania Chiki Mchomwa alisema kuwa uigizaji ni rasilimali muhimu sana na Tanzania ina waigizaji wengi na kama mipango ikikaa vizuri inaweza kutoa ajira nyingi kwani sanaa ajira zake haina ubaguzi wa rika.
“Tukifanya kazi zetu vizuri tutakuwa tumemsaidia mno Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, tunamshukuru sana yeye pamoja na Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa kuendelea kutoa ushirikiano na kuwa pamoja nasi nyakati zote. @michuzijr
@cloudsfmtz @filamu_tanzania @swahilitimes @tbc_online @habarileo_tz @tanzania_film_board @millardayo @dodoma_tv @dodoma_zone_ @